(Picha na Consolata Evarist.)
Mashindano ya Doto cup 2017 yamemalizika huku timu ya
Runzewe Academy ikiibuka na ushindi wa matuta zidi ya timu ya Chui FC.
Michuano hiyo ambayo inaandaliwa na Mbunge wa jimbo
la Bukombe mkoani Geita Doto Biteko kwa
lengo la kuibua vipaji husuani kwa vijana yalianza kutimua vumbi mwezi wa tisa
huku timu 45 zikishiriki kwenye mashindano hayo.
Akizungumza na mtandao wa maduka online ,Kocha wa Runzewe academy
Ramadhani Mgoi alisema kuwa huu ni msimu wa pili wa mashindano hayo na kwamba
wao ni mala ya pili wanachukua Kombe hilo na kwamba njia ambazo
wanatumia kupata ushindi ni kujituma kwenye mazoezi na wachezaji kuwa na
nidhamu.
Hata hivyo Kocha Mgoi ameobgeza kwa kumshukuru Mbunge kwa
kuendelea kuwa karibu na vijana na kuibua vipaji kwenye Wilaya hiyo.
Katibu mkuu wa baraza la michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja
ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye fainali hizo amehaidi
mwakani kufanya mabadiliko ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja
na kuleta wataalamu ili wawachague wachezaji kuchezea timu ya Taifa.
“ Ili mashindano haya yaweze kufanikiwa nilazima wapunguze umri wa
wachezaji kutoka miaka 15 mpaka 17 na pia natoa wito kwa halmashauri zote
zilizopo nchini kutenga maeneo ya michezo kwasababu
michezo ni ajila hivyo tukiwa na viwanja vingi kwanza vitasaidia
mapato kwenye halmashauri husika”Alisema Kiganja.
Kwa upande wake Mwandaaji wa michuano hiyo ,Mh Doto Biteko alisema
kuwa matarajio ni kuona vijana wa Wilaya ya Bukombe wanatoka kwenye michezo na
kufika nafasi ya juu zaidi ikiwa ni pamoja na kutoa timu ambayo itapanda daraja
na kuchenza fainali kubwa zinazoendelea hapa Nchini.
Imeandaliwa na Mtandao wa Maduka Online.
|
0 comments:
Post a Comment