METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, December 30, 2017

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI AFUNGA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU, KATA TATU

NA COMRADE EGOBANO

Leo jioni M/kiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini ndugu *Abubakari Mukadamu* akiongozana na katibu wa CCM wilaya , Mwenyekiti wa vijana wa mkoa na katibu wa vijana wa wilaya ya Shinyanga Mjini , wamehitimisha mashindano ya mpira wa miguu yaliyokuwa yakiendelea katika kata ya Old Shinyanga , ambapo pamoja na mambo mengine m/kiti alisisitiza kwamba mashindano haya yatakuwa endelevu kupitia jumuiya za vijana kata mbalimbali lengo likiwa ni kuwainua vijana kupitia vipaji walivyo navyo pia m/kiti aliwataka vijana kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kumuunga mkono Raisi wetu mpendwa wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

M/kiti wa Chama wilaya ya Shinyanga Mjini aligawa zawadi zilizokuwa zimeandaliwa kwa washindi wote baada ya mpambano kuwa mkali na kuibuka wao washindi, ambapo mshindi wa kwanza alipata Mbuzi wawili na Sh 30000 na mshindi wa pili akapata mbuzi mmoja na sh 20000 , Mshindi wa TATU akapata pesa Tasilimu Sh 30000 .

Haya yalikuwa ni mashindano yanayousisha kata Tatu za wilaya ya Shinyanga Mjini ikiwa ni mwendelezo wa kufanya mashindano mbalimbali ya vijana katika wilaya ya Shinyanga Mjini.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com