METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, December 30, 2017

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AIPONGEZA ILEMELA

Katibu mkuu wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto  Mhe Dkt Mpoki Ulisubisya ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Ilemela kwa kitendo chake cha ujenzi nafuu wa majengo ya zahanati ya Karume ukihusisha mafundi wazawa ikiwa ni utekelezaji wa lengo la Serikali la kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na mtoto

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake aliyoifanya hospitalini hapo mara baada ya kukagua majengo ya kutolea huduma za mama na mtoto likiwemo jengo la kuhifadhia maiti, jengo la upasuaji, jengo la maabara na nyumba ya watumishi

‘..  Niwapongeze kwa ujenzi bora na wenye gharama nafuu mliotumia mafundi wenu wa ndani  na kama mnavyojua Mheshimiwa Rais John Magufuli ameweka juhudi kubwa sana katika kuhakikisha Serikali inaboresha huduma za afya, na hili limemtofautisha yeye binafsi kama mfanya kazi kwa bidii sasa ni kwa nini na sisi kila mmoja wetu asiwe kama yeye?, …’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Mpoki amesisitiza juu ya kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya malaria huku akiitaka Ilemela kuwa manispaa ya mfano kati ya  manispaa zote zilizo kando ya Ziwa Viktoria kwa kuwa na mafanikio makubwa katika mapambano ya udhibiti wa ugonjwa wa kipindupindu

Kwa upande wake muwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt Silas Wambura amefafanua juu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na mkoa wake katika kuhakikisha huduma za afya zinaimarika na kupunguza vifo vya mama na mtoto

Akihitimisha kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga, mchumi wa manispaa hiyo Amosi Zephania amemuhakikishia katibu mkuu huyo wa wizara ya afya kutekeleza ushauri na maelekezo yote aliyoyaacha mbali na kupokea pongezi alizozitoa kufuatia juhudi za manispaa yake katika uboreshaji wa huduma za afya

Ikumbukwe kuwa kabla ya ujio huu Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambae pia  ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula alipata fursa ya kuzuru eneo la ujenzi huo na kusisitiza juu ya ushirikishwaji wa wananchi na utumiaji wa mafundi wazawa kwa gharama nafuu

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

30.12.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com