METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, December 31, 2017

BENKI YA DTB YAUNGANA NA ILEMELA KUMUUNGA MKONO MAKAMU WA RAIS JUU YA UTUNZAJI NA UHIFADHI MAZINGIRA

Benki ya Diamond Trust Bank DTB mkoa wa Mwanza imeungana na Halmashauri ya manispaa ya Ilemela katika kumuunga mkono makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu juu ya Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira kwa kufanya Usafi, kugawa miche elfu Tatu na mia tano  na kisha kuipanda miche hiyo kuzunguka uzio wa manispaa ya Ilemela, hifadhi ya barabara ya Buwelu kuelekea wilayani na viwanja vya manispaa tukio lilipambwa na kauli mbiu ya ‘ MAZINGIRA YETU, MAISHA YETU ’

Akizungumza katika tukio hilo mgeni rasmi na mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa tukio la ufanyaji usafi, upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa Ilemela limekuwa tukio endelevu kwani hata siku ya  kuzinduliwa kwa uzio wa manispaa hiyo na makamu huyo wa Rais alisisitiza na kuelekeza kutunza mazingira na kupanda miti huku yeye mwenyewe akianza kwa kupanda mti ndani viwanja ya manispaa huku akiwashukuru Benki ya DTB kwa namna walivyojitoa katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kulindwa sanjari na uoteshaji wa miti mipya waliyoitoa

‘… Ndugu zangu mtakumbuka siku ya uzinduzi wa ujenzi wa uzio wa halmashauri hii Mhe Makamu wa Rais alisisitiza pia juu ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti nayeye mwenyewe alipanda mti kama ushahidi kwa hiyo jambo tunalolifanya leo ni kuendeleza kile ambacho amekuwa akikisimamia kama mlezi na hivi karibuni pale Dodoma eneo la mzakwe amezindua kampeni ya kubadili hali ya mazingira, Kwetu sisi ni namna ya kuendeleza mazingira yetu na bahati nzuri wenzetu wa DTB Benki wamejitokeza na tumekubaliana nao mpango huu tutakuwa tukiuendeleza mwaka hadi mwaka …’ Alisema

Aidha tukio hilo pia lilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Kange Lugola ambapo amewataka wananchi kuacha kukata miti kwa kisingizo cha kupata nishati ya mkaa huku akiwaasa juu ya utumiaji wa nishati mbadala iliyorafiki wa mazingira mfano wa gesi sanjari na kuelezea hatua mbalimbali Serikali inazozichukua kupambana na uharibifu wa mazingira nakuzitaka halmashauri zote nchini kuzisimamia sheria za mazingira na uimarishwaji wa kamati zake kwa ngazi zote na kuahidi kuitembelea tena Ilemela mapema Januari, 2018

Nae mwakilishi kutoka Benki ya DTB Ndugu Sylvester Bahati amesema kuwa Benki yake imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kusaidia wananchi kwa  kutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za afya na Elimu hivyo zoezi la utoaji na upandaji miti ni muendelezo wa utoaji wa huduma kwa jamii kama inavyofanya maeneo mengine huku akiahidi kuendeleza mpango huo kwa kushirikiana na manispaa ya Ilemela

Akihitimisha mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga ameeleza juu ya umuhimu wa kutunza mazingira huku mkurugenzi wake John Wanga akiahidi kutekeleza maelekezo yote waliyoyatoa juu ya utunzaji mazingira na kushukuru kwa ushiriki wa viongozi hao katika zoezi hilo la kuhakikisha mazingira yanatunzwa

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com