Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akimimina mafuta ya taa kabla ya zoezi la kuteketeza nyavu
zinazotumika katika uvuvi haramu mjini Kigoma leo. Nyuma yake ni baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma watumishi wa umma na wanahabari
wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma leo.
Nyavu zinazotumika katika uvuvi
haramu zenye dhamani ya shilingi milioni 31 zikiteketea kwa moto
kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu nchini.
…………………………………………………………………………..
NA. MWANDISHI MAALUM KIGOMA
Waziri wa Mifugo na uvuvi Luhaga
Mpina ameteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu zilizokamatwa
mkoani Kigoma zenye thamani ya shilingi Milioni thelalini na moja
kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi hilo katika serikali hii ya awamu ya
tano.
Akiongea mara baada ya kuteketeza
nyavu hizo hizo mapema leo, Mpina alionyesha kushangazwa na suala la
uvuvi haramu kuwa sugu “kwa nini vita hii haina mwisho? Lazima
yawezekana mbinu zinazotumika ni dhaifu ama silaha zinazotumika ni duni,
ifike mahala suala hili liwe historia”. Alisema Mpina.
Akitoa Maelekezo kwa viongozi wa Mikoa ambayo shughuli hizi zinafanyika, Mpina aliwataka viongozi hao wawe na jukumu la kulinda rasilimali za taifa ikiwa ni mapoja na Bahari, Maziwa na mito.
“kama nitashindwa kushughulia
suala zima la uvuvi haramu, niitaaachia dhamana hii niliyopewa na
Mheshimiwa Rais, na mpaka kufikia hatua hiyo lazima wengi watakuwa
wamejuruhiwa.” Alisisitiza Mpina.
Akiwa katika ziara ya Oparesheni
Maalum ya Ondoa Mifugo kutoka katika mikoa ya mipakani na nchi jirani
akiwemo Mkoani kigoma, Mpina Pia alitembea mwalo mpya wa Kibirizi Mjini
Kigoma na kumtaka Afisa Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kigoma kushughulikia changamoto za mitambo wa kugandisha barafu
inayokikabili kikundi shirikishi cha rasilimali za uvuvi mwaloni hapo
pamoja na suala la kuwauzia dagaa wafanya biashara wanaozisafirisha nje
ya nchi. Waziri Mpina Pia alitembelea chuo uvuvi mjini Kigoma.
Zoezi la opareshini ondoa mifugo
na kukomesha rasmi uvuvi haramu limeanza rasmi kwa viongozi wa Wizara
husika wakiongozwa na mawaziri Luhaga Mpina na Abdalah Ulega kuingia
kazini katika mikoa inayokabiliwa na changamoto hizo.
0 comments:
Post a Comment