METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 27, 2017

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy avunja bunge la Catalonia

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy, anasema analivunja bunge la Catalonia na kuitisha uchaguzi wa mapema baada ya eneo hilo kujitangazia uhuru.
Waziri mkuu alisema kuwa udhibiti kamili kwa eneo hilo ni muhimu katika kurejesha hali ya kawaida.
Anamfuta kazi kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont na baraza lake la mawaziri
Mapema bunge la Catalonia lilipiga kura kwa wingi kujitangazia uhuru.
Mzozo huu ulianza wakati watu wa Catalonia waliunga mkono uhuru kwenye kura iliyokumbwa na utata mapema mwezi huu.
Bwana Rajoy alitoa tangazo hilo kufuatia masuala kadha ya siku nzima kuhusu uhuru wa Catalonia.
Bunge la Senate la Uhispania liliipa serikali ya Bw. Rajoy mamlaka ya kikatiba kufuta uhuru wa Catalonia na baada ya mkutano wa baraza la mawaziri Bw. Rajoy alisema kuwa hilo litafanyika
Catalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya watu walioshiriki katika kura hiyo asilimia 90 waliunga mkono uhuru.
Lakini mahakama ya katiba nchini Uhispnaia imeitaja kura hiyo iliyo kinyume na sheria.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com