Umoja
wa Mataifa (UN) umetoa Dola 160 milioni za Marekani kati ya Dola 200
milioni zinazitakiwa kutolewa mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza miradi
ya maendeleo ikiwamo kuwahudumia wakimbizi waliopo kambi mbalimbali
Kigoma.
Nusu
ya fedha hizo zimeelekezwa kwenye mradi wa Kigoma wa kuwahudumia
wakimbizi na kiasi kingine kimeelekezwa kwenye miradi mingine ya
maendeleo inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali ya UN.
Oktoba
24, UN itaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe za
maadhimisho hayo kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 500
wakiwamo na mabalozi, wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu
wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji
Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.’
Akizungumzia
maadhimisho hayo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, kimataifa na kikanda, Dk Susan Kolimba alisema
wameamua kuunganisha kauli mbiu ya Serikali ya kuendeleza viwanda na
mpango wa UN wa kutekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mratibu
mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez alisema programu ya Kigoma imebuniwa ili
kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa huo na hasa kuzilenga jamii
katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.
0 comments:
Post a Comment