Rais
Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa
ajili ya miundombinu na kilimo ni lazima uende kwa pamoja kwa sababu
masuala hayo ni masuala mtambuka kwa maendeleo ya taifa lolote duniani.
Dk.
Kikwete amesema hayo jana wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya
Radio ya Umoja wa Mataifa jijini New York, nchini Marekani, baada ya
kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya
tabia nchi, miundombinu, kilimo na vijana yamejadiliwa.
Dk.
Kikwete amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya
kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa kwa kutumia
mbegu zisizo na ubora na kusababisha wakulima kukosa mavuno yenye tija.
"Ukiendeleza
kilimo unasaidia watu wengi sana na umasikini wa Afrika una sura ya
vijijini kwamba masikini wengi waliopo Afrika wapo vijijini na tatizo
kubwa la kilino ni kwamba tunatumia dhana za zamani jembe la mkono
linatumika zaidi kuliko mashine na mitambo, asilimia 4 tu ya kilimo
chetu tunatumia umwagiliaji na mvua ya mwenyezi Mungu, tatu kilimo chetu
hatutumii mbegu bora tunatumia mbegu za asili ambazo hazizalishi sana"
alisema Jakaya Kikwete
0 comments:
Post a Comment