Kila tarehe moja ya mwezi wa kumi, Dunia nzima huadhimisha siku ya wazee kwa lengo la kutambua na kuenzi mchango wao katika jamii.
Leo wazee wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wameungana na wazee wenzao kuadhimisha siku hii.
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera, maadhimisho haya yalifanyika katika ukumbi wa krasta uliyopo tunduru Mjini.
Akihutubia katika maadhimisho hayo, Dc Homera alisema serikali inatambua umuhimu wa wazee katika jamii na kila kijana anapaswa kutambua kuwa siku moja ataufikia uzee hivyo wazee wanapaswa waheshimiwe, watunzwe na kuenziwa.
Awali, akijibu risala ya wazee iliyo ainisha changamoto mbalimbali zinazo wakabili wazee wa wilaya ya tunduru, Dc aliwaomba viongozi wao waende kwa afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya tunduru ili waweze kupata ushauri wa kitaalamu kwa mradi wowote wanaotaka kuifanya.
Aidha, DC aliwahimiza wazee kuendelea kufanya miradi ya pamoja au binafsi ili waweze kuungana na Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Joseph Magufuli katika harakati za kujenga uchumi wa Tanzania.
Alitoa rai kwa halmashauri ya wilaya ya tunduru kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuwapa wazee kipaumbele katika kutoa huduma za afya na kuwajengea ofisi ya kisasa itakayokuwa na Huduma zote muhimu kwa ajili ya chama chao cha Wazee na Wastaafu wilaya ya Tunduru(CHAWATU).
Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani ilienda sambamba na Mhe. Homera kuwapa fursa wazee kumuuliza maswali mbalimbali yanayohusu maendeleo wilayani tunduru na aliyajibu yote kwa ufasaha.
Pia aliwaomba viongozi wa chama cha wazee na wastaafu wilaya ya tunduru (CHAWATU) kuendelea kuwaleta wazee pamoja, swala la serikali kuwapa pensheni lipo kwenye ilani ya CCM 2015-2020 hivyo litatekelezwa muda wowote ni swala la kuwa na subira.
0 comments:
Post a Comment