Watanzania wakishangilia na kucheza
katika JAMAFEST aliyevaa safari suti ni Naibu Balozi wa Tanzania
nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko.
Aliyesimama na kushika Microphon Bw.
Iddi Suwed Mkurugenzi Mkuu wa Kikundi cha taifa cha tarabu cha Wizara
ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar wakati wakitumbuiza
nchini Uganda.
Wasanii wa kikundi cha Taifa cha Wizara Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar wakicheza ngoma ya asali ya Zanzibar.
Aliyevaa suti ya bluu na skafu ya
bendendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanania ni Kaimu Balozi ambaye
pia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko,
aliyevaa shati jeupe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel wa Naibu
Katibu Mkuu wake Bi. Nuru Milao wakiangalia ngoma za utamaduni katika
unoesho la usiku.
Baadhi ya Watanzania wakiangalia ngoma za utamaduni wakati wa onesho la sanaa usiku
Wasanii wa kikundi cha Kakau Band kutoka Bukoba wakitumbuiza katika jukwaa la Tanzania wakati wa mchana.
Wasanii wa kikundi cha Taifa cha
Utamaduni cha Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar
wakicheza ngoma ya Msewe ambayo ni maafuru Kisiwani Pemba.
……………………
KAMPALA
Tamasha la Sanaa na Tamaduni la Jumuiya
ya Afrika Mashariki JAMAFEST limeanza rasmi jana katikati ya mji wa
Kampala kwa wasanii wa sanaa za ubunifu za ngoma za utamaduni kwa
kuoneshwa bidhaa zao mbali mbali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Katika jukwaa la Tanzania Kikundi cha
Taifa cha Utamaduni cha Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
cha Zanzibar, Jinogile Band, Kakau Band na kikundi cha Taarabu cha
Taifa cha Zanzibar vilitia fora na kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi
waliofika katika Tamasha hilo.
Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya
ya Afrika Mashariki linatarajiwa kufunguliwa rami leo na Rais wa Uganda
Kaguta Yoweri Museveni katika viwanja vya Kololo na kauli mbiu ya
Tanasha hili ni Utamaduni na ubunifu wa viwanda ni injini ya umoja na
ajira
JAMAFEST ni tamasha lenye lengo la
kuwaunganisha wasanii wasanaa za ubunifu za utamaduni kwa kutafuta soko
la bidhaa hiyo adimu yenye wazalishaji wengi katika nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambayo inakuza sekta ya utalii katika Jumuiya na kwa
mwaka huu Tanzania imewakilishwa na washiriki zaidi ya 200.
Washiriki wa Tanzania katika maonesho ya
jana kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Kaimu Balozi ambaye pia ni
Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko, Mshauri wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Mambo ya
Utamaduni na Utalii Mhe. Chimbeni Kheri, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante
Ole Gabriel wa Naibu Katibu Mkuu wake Bi. Nuru Milao pamoja na Watanzana
wanaoishi na kusoma nchini Uganda.
Washiriki wa Tanzania wamekuwa na lengo
la kuonesha bidhaa ngoma za utamaduni, nguo, shanga, dawa za
mitishamba, lugha ya kiswahili, vyakula, mapishi na ulimbwende.
Habari na Picha
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
0 comments:
Post a Comment