METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 1, 2017

DKT MABULA ASHAURI KUWA NA UDHIBITI WANYAMA PORI WANAOINGIA KWENYE MAKAZI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameishauri Kuwa na namna bora ya kudhibiti wanyama pori wanaoingia katika makazi ya Wananchi ili kuepusha vifo na madhara mengineyo yanayoweza kujitokeza

Mhe Dkt Angeline Mabula ameyasema hayo akiwa hospitali ya rufaa Bugando mkoani Mwanza alipokwenda kuwatembelea majeruhi watano wakiwemo askari wawili kutoka idara ya wanyamapori Godwin Kambuga na Godfrey Haule , askari polisi wawili Yusuph Amir na  Otienel  mwihomeke  pamoja na  raia mmoja  Frank James  waliojeruhiwa na Chui  usiku wa kuamkia leo eneo la mtaa wa Kabangaja kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela

Akiwa hospitali hapo Dkt Angeline Mabula ameitaka Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kuchukua hatua za haraka kumdhibiti Chui huyo huku akiwaasa wananchi wa eneo hilo kuwa makini kipindi hiki cha uvamizi wa Chui huyo

‘… Nitoe tahadhara kwa wananchi wanaoishi katika eneo lile kuwa makini zaidi kwa sababu Chui huyu anawatoto na ameshajeruhiwa hivyo anahasira zaidi sasa akikutana na binadamu wengine anaweza kuwazuru tena, Lakini rai yangu nyengine ni watu wa maliasili kuanza kufuatilia Chui huyu katokea wapi kama ni kumrudisha alipokuwa au vinginevyo ili asilete madhara zaidi …’  Alisema

Kwa upande wake Askari polisi kutoka kituo cha Polisi Kirumba wilaya ya Ilemela Yusuph Amiri aliyenusurika kifo kutokana na kujeruhiwa na Chui huyo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula kwa kuwatembelea majeruhi wote na kuwasaidia huku akisimulia tukio zima la uvamizi wa Chui huyo na kujeruhi.

Akihitimisha muuguzi wa zamu kutoka hospitali ya rufaa Bugando walipolazwa majeruhi hao Bi Lucia Msombwa amesema kuwa majeruhi walipokelewa hospitalini hapo usiku wa kuamkia leo kufuatia kujeruhiwa vibaya na Chui huyo mmoja akiwa mahututi, mwengine akivunjika mguu, na waliobaki wakijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili na mpaka sasa amebaki mmoja anaendelea na matibabu wengine wakiruhusiwa kurejea nyumbani baada ya matibabu.

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
01.09.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com