METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 25, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA VODACOM MSIMU WA 2017/18

Photo 1
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (katikati)akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
Photo 2
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro akiongea na waandishi wa habari (hawapop ichani) wakati wa hafla hiyo.
Photo 3
Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia akiishukuru benki ya KCB Tanzania kwa udhamini huo.
Photo 4
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (aliyekaa Kulia)na Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (aliyekaa kushoto)wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi 325,000,000 uliotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa TFF.Pamoja nao wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (aliyesimama kulia), Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (aliyesimama katikati) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (aliyesimama kushoto).
Photo 5
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Cosmas Kimario (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Zuhura Muro (wa pili kulia) wakikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 325,000,000 kwa Raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia (wa pili kushoto), ikiwa ni udhamini kwa ajili ya ligi kuu ya soka ya Vodacom 2017/18. Pamoja nao kwenye picha ni Makamu wa Raisi wa TFF Michael Wambura (wa kwanza Kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao (wa kwanza kushoto).
Photo 6
Bodi ya Utendaji wa ligi kuu kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya KCB Tanzania na shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Photo 7
Menejimenti ya benki ya KCB Tanzania kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Photo 8
Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya KCB Tanzania.
…………………

Dar es Salaam, September 2017 – Benkiya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi ya soka ya TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania 325,000,000.Mkataba wamakubaliano hayo ulisaini wa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF Wallace Karia.

Hafla hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi,Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi ya Udhamini TFF,  Mhe, Mohammed Abdulaziz, Wakurugenzi wa Bodi ya KCB Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania, wawakilishiwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubw akatika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini,hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiungana TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu” alisema Kimario.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema kuwa“Benki ya KCB Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kw wapenzi wa mpira wa miguu na kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya maendeleo kw abenki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi kwa ujumla.

Raiswa TFF aliishukuru benki ya KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Kuhusu Benki ya KCB

Benkiya KCB ni benki kubwa zaidi katika Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benk iya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. 

KCB Bank Group pia lina miliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.

Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 natoka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania barana visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugujijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main naTFA, MwanzanaMorogoro.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la AfrikaMashariki
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com