Mkuu wa Skuli ya Uunguzi na Ukunga Chuo
Kikuu cha Aga Mjini Nairobi Kenya Khan Prof. Sharon Brownie akizungumza
na viongozi wa wauguzi na wakunguga wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja
akisisitiza juu ya kuinua na kuimarisha kada hiyo kupitia Jumuia zao.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wauguzi na
Wakunga Zanzibar Bi. Amina Abdulkadir akitoa ufafanuzi kuhusu Jumuia
hiyo inavyofanyakazi na kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi wa kada hiyo
kujiendeleza katika mkutano huo uliofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Mmoja wa viongozi wa wauguzi Bi. Salama Rashid Haroub akitoa mchango wake juu ya kuikuza kada ya uuguzi na ukunga Zanzibar.
Baadhi ya viongozi wa Wauguzi na Wakunga
wakifuatilia mkutano mkutano huo uliohutubiwa na Mkuu wa Skuli ya
wakunga na wauguzi kutoka chuo Kikuu cha Aga Khan Mjini Nairobi Kenya.
Picha ya pamoja ya viongozi wa wauguzi
na wakunga wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wauguzi Zanzibar na
wageni wao kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi Kenya ambapo wamekuja
Zanzibar kuinua kada ya wakunga na wauguzi.Picha na Makame Mshenga.
Na Miza Kona Maelezo-Zanzibar
Wauguzi na Wakunga nchini wamesisitizwa
kuongeza bidii katika kuongeza taaluma katika fani yao kwa lengo la
kutoa huduma kwa ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Hayo yameelezwa leo huko Hospitali ya
Mnazi Mmoja na Mkuu wa Skuli ya Wauguzi na Wakunga wa Chuo Kikuu cha Aga
Khan nchini Kenya Profesa Sharon Brownie alipokuwa akizungumza na
wasimamizi wa wauguzi na wakunga wa Hospitali hiyo.
Prof. Sharon amesema wauguzi wana nafasi
muhimu kwa jamii hivyo ni vyema kutafuta ujuzi kupitia sehemu nyengine
kwa lengo la kukuza fani hiyo.
“Asilimia 90 ya wauguzi duniani ni
wanawake, wauguzi mnatakiwa kuangalia mitandao ya wauguzi ambayo inatoa
taaluma ya uuguzi kufanya hivyo mtaweza kubadilika kifanisi katika kazi
hii ya uuguzi,” alieleza Profesa Sharon
Alifahamisha kuwa fani ya uuguzi
inatakiwa kufanyakazi kwa kujituma na mashirikiano katika utendaji na
utoaji huduma na kuweza kuinua afya kwa jamii
Alieleza lengo la ziara hiyo ni kuinua
na kuboresha Wauguzi pamoja na Jumuiya za Wauguzi kwa dhamira ya
kuendeleza kitaaluma na kutekeleza majukumu ya kazi hiyo kwa ubora
pamoja na kuimarisha afya kwa jamii.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wakunga na
Wauguzi Bi Amina Abdulkadir amewataka wasimamizi pamoja na wauguzi
kufanya kazi kwa kujiamini, kujiheshimu pamoja na kubadilika kifanisi na
kujua majukumu ili kuweza kutekeleza majukumu yao bila ya katawaliwa na
kudharauliwa na wengine.
“Muuguzi anatakiwa kufanya kazi kwa
kujiamini, awe smati, ajiheshimu pia anatakiwa kubadilika kielimu sio
awe regerege awe ni mwenye kufanya maamuzi ndio mfanyakazi mwengine nae
atamuheshimu, sisi tunataka wauguzi muwe juu zaidi katika fani hii,”
alifahamisha Bi Amina.
Aidha Bi Amina amewasisistiza wauguzi
hao kuipenda kazi yao kwa lengo la kutoa huduma iliyo bora kwa jamii ili
kuepukana na usumbu na malalamiko yanayotolewa na jamii.
Nao wauguzi hao walisema wanafanyakazi
katika mazingira magumu hivyo wanahitaji kupatiwa elimu na vifaa vya
afya ili waweze kujiimarisha zaidi na kutoa huduma bora kwa jamii.
Aidha wauguzi hao walisisitiza kufanya
utafiti katika kazi zao ili kuweza kujua na kupata sababu zinazoikumba
jamii wakati wa utoaji huduma kwa lengo la kuimarisha afya na kuepukana
na changamoto zinanajitokeza.
0 comments:
Post a Comment