Watafiti wa zao la korosho wametakiwa kuunganisha utafiti na masoko ili kuwasaidia wakulima wakati wa uongezaji wa thamani ya mazao yao
Akiongea wakati alipotembelea mabanda ya Kituo cha utafiti cha Naliendele Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt Charles John Tizeba amesema namna pekee ya kuwasaidia wakulima wa korosho ni kuwapa elimu juu ya teknolojia za usindikaji na uongezaji wa thamanai wa bidhaa zitokanazo na korosho na kuwaunganisha na masoko.
“mmekuwa mkifanya tafiti nyingi na kubwa kwa zao la korosho na mhogo sasa utafiti wenu usiishie kwenye kutafiti wa teknolojia za uzalishaji pekee lakini muweze kuwaunganisha wakulima soko na uongezaji wa thamani wa bidhaa zitokanazo na tafiti zenu.” alilisistiza Mhe. Tzeba.
Aidha amesema serikali imekuwa ikijitahidi kutoa ruzuku za pembejeo na kufuta kodi ambazo zilikuwa ni kikwazo kwa wakulima lengo likiwa ni kumnyanyua mkulima mdogoWaziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Chales John Tizeba
0 comments:
Post a Comment