Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakimsikiliza Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka
Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM umewasihi Vijana kote nchini wanapaswa kutumia Maskani zao kwa hamasa ya shughuli za Maendeleo yao na kukuza uchumi katika Jamii.
Umoja huo umeonya Vijana kutumia Maskani kwa kupiga sogo za kisiasa pasina kufanya kazi Jambo ambalo linapelekea kwa Wakati wote kuilaumu Serikali ilihali walipaswa kutumia weledi wao kuanzisha vikundi Mbalimbali vya kijamii ambavyo vingewaongezea kipato.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati alipotembelea na kuwasalimu Vijana wa Maskani ya Subira yavuta kheri iliyopo eneo la Mgogoni Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Ili kubaini changamoto zao na kushirikiana namna ya kutatua.
Alisema kuwa kuanzisha Maskani Ni jambo zuri Kama Vijana watashauriana namna ya kujikwamua kimaisha kwa kufanya shughuli zao Mbalimbali za kijamii zitakazoshika kipato ikiwa Ni pamoja na Kujiunga na vikundi vya ujasiriamali.
Pia aliwasihi Vijana hao kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli sambamba na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohamed Shein kwani wana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wanachi kwa weledi Mkubwa.
Shaka Alisema kuwa Ni vyema kuwasaidia Vijana waliojiunga na vikundi mbalimbali kupata mikopo serikalini lakini busara zaidi Ni kuwasaidia kwa kuwapatia ujuzi katika nyanja Mbalimbali ikiwa Ni pamoja na Kujifunza mbinu Bora za Ufugaji na Kilimo sambamba na namna ya kuwa na nidhamu ya fedha ili kupitia ujasiriamali wawe na mafanikio makubwa.
Alisema kuwa ili kuwa na Vijana makini katika Jamii UVCCM imeamua kukifufua Chuo Cha Siasa Uongozi, Itikadi na Ujasiriamali kilichopita Kijiji cha Ihemi Mkoani Iringa ambapo Vijana Mbalimbali watapata fursa ya kujifunza mambo muhimu na muhimili katika Jamii.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment