Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Uongozi
mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umetakiwa kufikia
Januari mwakani kuwajibika kama mashirika mengine ya mpira wa miguu
duniani yanavyowajibika kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye
magazeti ili wananchi wapate fursa ya kufahamu namna fedha
zinavyopatikana na jinsi zinavyotumika katika kuboresha na kuendeleza
usimamizi bora wa soka nchini.
Rai
hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jana katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani
Dodoma
Aidha
Mhe. Mwakyembe aliwapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza TFF
kwa muda wa miaka minne kwa kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na
kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku huku akiwapongeza
washiriki wote waliothubutu kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali
wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF wa mwaka huu.
Kwa
upande wake Rais mpya wa TFF Bw. Wallace Karia amewaahidi wapiga kuwa
wake kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwani nafasi aliyopewa na
wajumbe hao kwa kumuamini ni deni ambalo atalilipa kwa kuleta mafanikio
makubwa katika mchezo wa soka.
Bw.
Karia alisema kuwa furaha waliyonayo viongozi wote waliochaguliwa
kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne iende kuwa furaha ya kazi kwa
kufanya yale watanzania wanatarajia kutoka kwao.
0 comments:
Post a Comment