Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Magufuli na Rais
mstaafu wa Marekani, Barack Obama ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa
kuhudhuria katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Kenya, Uhuru
Kenyatta.
Kamati
ya maandalizi ya sherehe hizo inayoongozwa na Katibu Kiongozi, Joseph
Kinyua imebainisha kuwa imeandaa orodha ya majina ya viongozi wa
kimataifa kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria la uapisho wa
Kenyatta endapo ushindi wa Kenyatta hautopingwa mahakamani.
Kwa
mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, sherehe za uapisho hufanyika siku 14,
baada ya mshindi wa uchaguzi kutangazwa ili kutoa fursa kwa chama
chochote kinachotaka kupinga matokeo kufanya hivyo.
Viongozi
wengine wanaotarajiwa kualikwa katika sherehe hizo wakiwemo wakuu wa
nchi ni pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri
Museveni, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa Nigeria Muhammadu
Buhari. Wengine ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa
Uingereza Theresa May.
Aidha,
katika orodha hiyo pia yupo Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf,
mfanyabiashara tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote, Kiongozi wa
Jumuiya ya Ismailia, Aga Khan, Waziri Mkuu mstaafu wa Italia, Matteo
Renzi na Rais Xi Jinping wa China.
“Tupo
kwenye maandalizi ya sherehe za uapisho wa Rais wakati tukisubiria
hatua za kikatiba kukamilika. Orodha hii ni ya marafiki wa Kenyatta,
viongozi wa Afrika na viongozi wengine wa kimataifa, tunaotarajia
kuwaalika”, amesema mmoja wa wanakamati hiyo ya maandalizi.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi Kenya, Wafula Chebukati mwishoni mwa
wiki alimtangaza rasmi Rais Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kuwa
washindi katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita nchini humo.
0 comments:
Post a Comment