Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na wawakilishi wa Taasisi mashirika mbalimbali (Hawapo pichani)
zilizochangia wanananchi wa Bukoba Mkoani Kagera waliopatwa na maafa ya
tetemeko la ArdhiSeptemba 10 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu amepokea fedha
taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni
mbili kutoka kwa wadau mbalimbali, Huku Shirika la Madini la STAMICO
likichangia jumla ya shilingi milioni 20 katika fedha hizo.
Fedha
hizo jumla ya shilingi milioni 20 zilizotolewa na STAMICO ni michango ya
pamoja iliyotolewa na kampuni tanzu za KTCL, SAMIGOLD na STAMICO
yenyewe.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam leo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-MAGOGONI DAR ES SALAAM)
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi
akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wao wa shilingi milioni 20 kwa
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kulia kwake ni Mahende Michael Peter
Mwanasheria Mkuu wa STAMIGOLD na waliosimama nyuma kutoka kushoto ni
Raymond Rwehumbiza Mratibu wa mradi Ununuzi wa Madini ya bati KTCL
uliopo Kyerwa Mkoa wa Kagera, Alex Rutagwelela Kaimu Mkurugenzi wa
Uchorongaji STAMICO , Beatrice Musa Lupi Mhasibu Mkuu STAMICO na Koleta
Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma STAMICO.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi
akimuonyesha Waziri Mkuu Vocha ya malipo yaliyofanywa kwenye akaunti ya
kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi Kagera kabla ya kukabidhi rasmi
kwa waziri mkuu kutoka kushoto ni Mahende Michael Peter Mwanasheria na
Mkuu wa Kitengo cha Sheria STAMICO na Koleta Njelekela Meneja Masoko na
Uhusiano kwa Umma STAMICO.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini nchini STAMICO Bi.Zena Kongoi
akikabidhi vocha hiyo kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kutoka kushoto
ni Raymond Rwehumbiza Mratibu wa Ununuzi wa Madini ya KTCL Kyerwa Mkoa
wa Kagera, Mahende Michael Peter Mwanasheria na Mkuu wa Kitengo cha
Sheria STAMICO na Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma
STAMICO.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipiga
picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Bi. Zena Kongoi na ujumbe
wake alioongozana nao kutoka shirika hilo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa aki
akizungumza jambo na Bi. Koleta Njelekela Meneja Masoko na Uhusiano kwa
Umma STAMICO mara baada ya makabidhiano hayo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa na wageni mbalimbali waliofika ofisini kwake kutoa msaada kwa ajili ya wahanga wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera wakimkubuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo chake miaka 17 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment