Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Ndg Raymond Mwalimu amewasihi vijana kuendelea kushiriki katika Michezo ili kujenga Afya zao sambamba na kujenga mshikamano kati Yao.
Nasaha hizo zimejili Wakati akizungumza na wachezaji wa timu zilizoshiriki Mashindano ya Nanenane Cup ambayo kusudio lake kubwa ilikuwa Ni kuunga mkono Maadhimisho ya Nanenane ambayo kikanda yamefanyika katika Mkoa wa Mwanza huku kitaifa yakiwa yamehitimishwa Katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Ndg Mwalimu amesisitiza zaidi mahusiano chanya baina ya Vijana katika Mkoa wa Mwanza Jambo ambalo litazaa matunda ya mafanikio na hatimaye kuachana na dhana ya kuilaumu Serikali pasina kujishughulisha.
Pia amekabidhi zawadi ya N'gombe kwa Timu ya MARSH Academy ambao ndio wameibuka washindi katika mchezo was was fainali kwa kuwachapa bila huruma timu ya Lumumba Fc.
Katika mechi hiyo ambayo Mshindi amekabidhi zawadi ya N'gombe imefikisha ujumbe kuwa sikukuu ya wakulima na wafugaji ina husisha pia Ng'ombe kwa ajili ya kulimia huku mnyama huyo pia Akitumika Kama kitoweo kwa nyama yake sambamba na ngozi ambazo zinatumika kutengeneza viatu.
Mashindano hayo yamemalizika katika viwanja vya nyamagana huku timu zilizoingia hatua ya Nusu Fainali siku ya tarehe 6, 2017 ikiwa ni Timu ya Millo FC, Uhuru FC, Marsh Academy na FC Lumumba.
Katika mechi hiyo ya Hatua ya Fainali mpaka dakika 90 za mchezo timu zote zilikuwa zimechoshana nguvu kwa kumalizia kwa sare ya magoli mawili kwa mawili ambapo ilipelekea kuingia Hatua ya kupiga penati na hatimaye Marsh Academy wakapata goli 4 na Fc lumumba wakapata goli 3.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment