Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitoa maelekezo kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Temani ambayo wana ghala la kuhifadhia
vinywaji aina ya viroba lililoko Kimara Temboni Bibi Elizabeth Massawe
(wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ghala hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa
Habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ghala la
kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani lililopo Kimara Temboni.
Sehemu ya vinywaji aina ya viroba na vifungashio vilivyopo katika ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amesema kuwa
Serikali haina mpango wa kutoa vibali kwa ajili ya kuuza shehena ya
kinywaji aina ya viroba vilivyopo stoo kwenye maghala ya Wafanyabiashara
wa pombe hiyo.
Aliongea hayo jijini Dar es
Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika ghala la kampuni ya
usambazaji wa vinywaji aina ya kiroba ya Temani iliyopo Kimara Temboni
jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa Serikali ilitoa
muda mrefu kuanzia mei 2016 mpaka machi 2017 kwa wenye shehena hiyo ya
viroba kuuza na kumaliza mzigo wote uliopo stoo hivyo basi baada ya
Serikali kupiga marufuku pombe hiyo, hakuna kibali kitakachotolewa kwa
ajili ya kuuza shehena ya mzigo wa viroba uliobaki. Akiongea kwa Mh.
Waziri , Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bi Elizabeth Massawe alisema
wanaiomba Serikali iwasaidie ili waweze kupunguza mzigo mkubwa wa viroba
ambao wanao katika ghala lao sababu wanapata hasara kubwa na wanatakiwa
kulipia kodi ya magahala waliyokodi.
Katika ziara hiyo ya
kutembelea ghala la vinywaji la kampuni ya Tema Enterprise Waziri
alikuta shehena kubwa ya katoni 150,000 za viroba zilizofungashiwa
katika vifuko vya plastiki.
0 comments:
Post a Comment