METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 25, 2017

Dkt Rehema Nchimbi aagiza kuharakisha ukarabati wa uwanja wa Namfua

Siku chache baada ya wapenzi na mashabiki wa soka  Mjini Singida kuelezea hofu yao juu ya kutokamilika kwa Uwanja wa Namfua na kutumiwa na Singida United kwa michuno ya ligi kuu Tanzania bara, Serikali imeingilia kati na kuhakikisha kuwa shughuli za ukarabati zinaanza kufanyika.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema shughuli za ukarabati huo sasa zitafanyika usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa uwanja huo wa Chama Cha Mapinduzi unakamilika kabla ya Agosti mwaka huu.

-Kwa gharama yoyote ile, na hata ikilazimika kufanya kazi usiku na Mchana ni lazima uwanja huu ukamilike mapema na uweze kutumiwa na Singida United kama uwanja wao wa Nyumbani msimu ujao wa Ligi kuu” Nchimbi alisema.

*Uzembe umefanyika.*

Msimamizi huyo wa Shughuli zote za kiserikali Mkoani Singida, amekiri kwamba kuna uzembe umefanyika katika kuukarabati uwanja huo, lakini amesema si wakati wa kumtafuta nani amekosea bali kujitahidi ili Singida United wautumie uwanja huo Kuanzia Agosti mwaka huu.

Kuna uzembe umefanyika lazima tukiri, lakini huu si wakati wa kutafuta nani amefanya amekosea, bali kutafuta namna ya pamoja ya kuweza kuukamilisha mapema na Uwanja huu uweze kutumika Msimu ujao na Singida United’ Aliongeza Nchimbi.

*Kila mdau.*

Katika Upande Mwingine Dkt Rehema Nchimbi ametoa wito kwa kila mdau wa michezo mkoa humo kutimiza wajibu wake ili uwanja huo uweze kukamilika kwa wakati, na kuanza kutumika kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

Singida United iliyoshuka daraja miaka 15 iliyopita, imebahatika kupanda tena msimu huu na inatarajia kutumia Namfua kama Uwanja wake wa nyumbani kwa michuano ya ligi kuu Tanzania bara.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com