METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 1, 2017

ZAIDI YA VIJANA 500 IRINGA WASHIRIKI KATIKA TAMASHA LA JPM STAR SEARCH

Wasanii chipkizi mkoani iringa wamewalalamikia wasanii wakubwa kwa kushindwa kuwapa ushirikiano katika kazi mbalimbali za sanaa hali inayochelewesha wasanii wadogo kufikia mafanikio na hivyo kudumaza tasnia hiyo hapa  nchini

Wakizungumza katika uzinduzi wa Tamasha linalojulikana kwa Jina la JPM Starsuch lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Manispaa ya Iringa na kufanyika katika ukumbi wa Hall Fear mkoani hapa kwa lengo la kibua vipaji mbalimbali kwa vijana  walisema kumekuwa na ugumu kwa wasanii wa kubwa kuonesha ushirikiano kwa wasanii wachangajambo linalosababisha linayosababisha kushindwa kuwepo kwa ushindani katika tasnia ya film na muziki na kuleta Tija kwa Taifa.

De Money ni miongoni mwa wasani chipkizi wa Sanaa ya Muziki wa Bongo Freva aliiambia SAYARI YA HABARI kuwa richa ya vijanawasanii kujiytuma lakini bado wanahitaji Sapoti kutoka kwa wasanii wakubwa jambo ambalo lipo tofauti kwani baadhi ya wasnii wakubwa wamekuwa wakihitaji fedha nyingi ili kufanya nao Korabo(kushirikisha)katika nyimbo kwa kisisngizio kwamba wanawabeba

“Tunatamani sana kufika mbali kwasababu kama masinii unapofanyakazi unakuwa na maono ya wapi unataka kufika lakini pia kama msanii unajaribu kuwatafuta wasanii waliotangulia angalau wanamajina lakini changamoto kubwa hawaoneshi ushirikiano wa moja kwa moja gharama inakuwa kubwa ukitaka umshirikishe katika nyimbo yako natamani tusaidiane tuitangaze sanaa yetu ya Muziki” Alisema Msanii huyo

Merina Mlowe pia ni miongoni mwa waigizaji walioshiriki katika uzinduzi wa Tamasha Hilo ambapo alisema kama wasanii wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa fedha kama mitaji kwaajili ya kufanyia kazi zao jambo linalokwamisha jitahada wanazozifanya katika kutengeneza Tamthilia zenye Ubora hivyo aliiomba serikali iwasaidie waweze kupata mitaji ili iwasaidie kuandaa kazi bora.

“Kwa kweli tunatamani sana kufanya kazi kwa kiwango kikubwa lakini tunashindwa kutokana na uhaba wa fedha ila tunawapongeza UVCCM kwa kuona waanze kuuanda mikakati ya kuibua vipaji na kuikumbusha serikali wajibu wake katika kutuwezesha vijana tuweze kujiari” Alisema Merina

Kwa upande wake  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba alisema wasanii wakubwa ili kuiinua sanaa Tanzania ni lazima wasanii wakubwa watumie nafasi zao kuwainua wasanii chipkizi  kwani ili sanaa iwe na Tija kwa Taifa ni lazima watu wengi wawekeze katika shughuli hiyo badala ya kuwakatisha tama na kushindwa kufanya kazi pamoja na wasanii hao wachanga.

“Hii ni kiongoni mwa changamoto ambazo zipo pengine mi mi nisema ni vema sasa wasanii wakubwa wanajitambua tena kwa majina ifike wakati tuwaone wasanii wadogo ni sehemu yetu hawa wakikua watatusadai lakini pia niwatie shime hilo lisiwakatishe tamaa kuweni wabunifu fanyeni kazi”alisema

Alphonce Myinga ni Katibu wa UVCCM Manispaa ya Iringa alisema Mashindano  hayo richa ya kuibua vipaji lakini pia yalilenga kuwakutanisha vijana pamoja ili kuoneshana wapi zinapopatikana Fursa ili vijana waweze kuwa na mambo ya kufanya badala ya kubaki wakilalamika kuwa hakuna ajira ipo haja kwa vijana kuanzisha miradi yao ikiwa nai pamoja na kujiingiza kwenye sanaa ili waweze kuonesha vipaji vyao na kuitangaza nchi.

“Kanuni za umoja wa vijana zinaniongoza mimi hasa nikiwa natekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini nimeandaa tamasha hili ili kuhakikisha tunawaunganisha vijana ili waepukane na matendo mabaya wawe na jambo la kufanya kwa sababu sanaa ni ajira wajibu wangu ni kuwa linda vijana ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.”alisema katibu UVCCM

Naye Mkuu wa Milaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alisema ipo changamoto kwa baadhi ya wasanii ambao hutumia nafasi zao kwa kudharau wengine na kuona wamefanikiwa jambo linalorudisha Nyuma maendeleo hivyo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza baadhi ya wasanii wenye nia ya kuwainua vijana wenzao ambapo kwa kwakufanya hivyo kunawafanya na wao kufanikiwa zaidi.

“Niwakumbushe wasanii nchini upo ukomo wa kuwa msanii hebu tumieni nafasi zenu kuwainua wasanii wenzenu kwani njia hiyo ndiyo hutumiwa na nchi zilizoendelea wale waliofanikiwa wanatumia nafasi zao kuwasadia waliochini ili kuweka Chain ya Wasanii mmoja anaposhindwa Yule aliyeibuliwa anaendeleza pale pongezi nyingi kwa Diamond kwa kusaidia vijana wenzake.” Alisema Kasesela

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com