Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo asubuhi
amekabidhiwa zawadi ya gari aina ya Double Cabin Wingle 5 kutoka kwa kampuni ya
watengenezaji wa magari ya Great Wall Motor ya Afrika Kusini ikishirikiana na
kampuni ya wauzaji wa magari ya Kifaru Motors ya Tanzania.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Great Wall
Motor Company ukanda wa kusini mwa Afrika Bwana Jianguo Liu alisema kuwa zawadi
hiyo ni ishara ya kampuni hiyo kutambua jitihada mbalimbali za Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa na watumishi wake wanazofanya katika kutumikia wananchi na kusaidia
kuboresha utendaji kazi.
Katika salamu za shukrani Mhe. Paul Makonda aliushukuru
Uongozi mzima wa Kampuni ya Great Wall
Motor ukishirikiana na wauzaji wa magari ya Kifaru Motors kwa kutambua jitihada
za Ofisi yake na kuahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salam
kwa moyo na kutimiza falsafa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ya “HAPA KAZI TU”.
Mkuu wa Mkoa ameahidi kuwa gari hilo litatumika ipasavyo
katika kuwahudumia wananchi wa Dar es Salaam na kutumiwa na Idara
itakayoonekana kuwa ndio mtoa huduma bora katika Mkoa wa Dar es Salaam.
“Naomba kuitoa hii gari kama zawadi kwa Idara inayohudumia
vizuri wananchi wangu na ili nitoe kwa Idara hiyo naomba wananchi wenyewe
watutumie kwa ujumbe mfupi kupitia namba tutakayoitangaza. Kazi ya wananchi ni
kusema tu Idara hii inawahudumia vizuri wanapofika kwenye ofisi zao,kama ni
Afya,Elimu,Ardhi,Biashara,na Mahakama”. Aliongeza Mhe. Paul Makonda.
Kwa mfano kama ulienda Idara ya Elimu, Ardhi, Afya, au
Biashara ukapewa huduma nzuri katika eneo mojawapo kati ya hayo unachotakiwa
kufanya ni kutuma mesesji fupi inayoonyesha Idara hiyo ili wapewe zawadi hiyo
ya Gari kama motisha ili waendelee kutoa huduma nzuri.
Utaratibu wa kutuma ujumbe huo wa kuchagua Idara bora katika
utendaji utatolewa kupitia namba maalum ambayo itatolewa hapo baadae.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Habari na Uhusiano
OFISI YA MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
05/07/2017
0 comments:
Post a Comment