METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 11, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AKABIDHI KOMPYUTA

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula leo ameikabidhi Shule ya Sekondari  Bugogwa jumla ya Kompyuta Ishirini ikiwa ni muendelezo wa jitihada zake katika kuhakikisha anaboresha Elimu Jimboni ili kupata wataalamu bora na wenye weredi wakutosha kuifikia Tanzania ya Viwanda zoezi lililohudhuriwa pia na madiwani wa Manispaa ya Ilemela.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule hiyo  kwa niaba yaTaasisi ya Christian Life World Mission Frontiers kutoka nchini Korea ya Kusini inayoshirikiana na Mbunge huyo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuishukuru Taasisi hiyo kwa  kuunga mkono jitihada anazozifanya katika kuleta Maendeleo amewaasa wanafunzi na walimu kuvitumia vizuri vifaa hivyo sambamba na kuvitunza  ili kufikia Tanzania ya Viwanda  kwa kuzalisha wataalamu bora na wenye weredi kukidhi soko la wakati.

‘… Niwaombe wanafunzi lakini pia walimu wangu kwa pamoja mvitumie huku mkijitahidi sana kuvitunza vifaa hivi ili tuweze kupata wataalamu bora na wenye weredi kukidhi matakwa ya soko la wakati la kuwa na nchi ya Viwanda, Tanzania ya Viwanda haiwezi kufikiwa kama hatujazalisha wataalamu wakutosha, Hivyo basi hii ikawe chachu  katika  kuifikia hiyo Tanzania ya Viwanda…’

Kwa upande wao Taasisi ya Christian Life World Mission Frontiers chini ya Rais wake Mchungaji Paul Kim mbali na kufurahisha na mazingira ya shule ya Sekondari Bugogwa ameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula huku akiongeza kuwa huu ni mwanzo katika kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ndani ya Jimbo hilo.

Wakihitimisha  walimu na wanafunzi wa shule hiyo wamemshukuru Mhe Mbunge  wa Jimbo la  Ilemela kwa jitihada zake za kuhakikisha anawaletea wananchi wake Maendeleo katika nyanja mbalimbali huku wakiahidi kuunga mkono Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt John Magufuli  yenye dhamira ya kweli katika kuwaletea wananchi maendeleo.

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
10.07.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com