METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 8, 2017

MBUNGE WA ILEMELA ASHIRIKI MAHAFALI YA 52 YA CHUO CHA MALIASILI PASIANSI

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula leo ameshiriki sherehe za mahafali ya kuhitimu  jumla ya wanafunzi 432  wa fani mbalimbali waliokuwa wakisoma chuo cha Maliasili na Wanyamapori cha Pasiansi wilayani Ilemela yaliyonogeshwa na kauli mbiu ya ‘ Hifadhi Wanyamapori kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda ’ huku Mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Prof Jumanne Maghembe

Akizungumza katika Mahafali hayo Mgeni Rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Jumanne Maghembe amewataka Majangili kuacha mara moja vitendo vya kijangili kwa kuwa vinachangia kudumaza uchumi wa nchi huku akiongeza kuwa Serikali haitavumilia vitendo vya namna hivyo na kuahidi kuwa watakaokaidi tamko hilo kukiona

‘… Tunayochangamoto kubwa ya kukabili majangili na kwa namna tunavyokwenda nataka niwatumie salamu majangili ya kuwaambia kazi hiyo waache vinginevyo waswahili wanamsemo wao wanasema watakiona chamtema kuni na hakuna mtu anayejua kilichompata mtema kuni kilikuwa ni nini??  …’

Aidha Mhe Prof Maghembe ametumia hadhara hiyo kumpongeza Mhe Rais Dkt John Magufuli kwa kauli yake aliyoitoa mapema alipotembelea wizara ya maliasili na utalii ya kukemea vitendo vya kijangili na kuasa kuchukuliwa hatua kwa mtu yeyote bila kujali dini yake, kabila lake, umaarufu wake, cheo chake au mali zake kama atajihusisha na vitendo hivyo

Akimkaribisha mgeni rasmi Dkt Angeline Mabula mbali na kuwapongeza wahitimu amewakumbusha wakazi wa Ilemela juu ya kuendelea kumuombea Mhe Rais Dkt Magufuli kwa hatua mbalimbali  anazozichukua kuhakikisha anawaletea wananchi wake maendeleo huku akiwataka kukaa teyari kufuatia ziara atakayoenda kuianza muda mfupi ikihusisha mrejesho wa kumalizika kwa vikao vya Bunge na usikilizaji wa changamoto sanjari na kuzipatia ufumbuzi na kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kulipa kodi za ardhi na umuhimu wa urasimishaji makazi

Akihitimisha sherehe hizo mkuu wa chuo hicho  Bi Lawaeli Damalu Ameishukuru Serikali kwa namna inavyoboresha taasisi hiyo siku hadi siku kufuatia uongezaji wa vifaa vya  kisasa vya kujifunzia na namna inavyotoa mafunzo shirikishi tofauti na ilivyokuwa hapo awali

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
08.07.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com