METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 4, 2017

MAFANIKIO YA MRADI WA BRT MWENDOKASI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NI MATOKEO YA UTEKELEZWAJI WA ILANI YA USHINDI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Ibara ya 39 ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 inaielekeza Serikali kutekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la DSM. Serikali ya Awamu ya Tano imekamilisha Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka  (BRT) katika Jiji la DSM iliyojumuisha barabara za Kimara-Kivukoni, Magomeni-Morocco na Fire-Kariakoo zenye urefu wa jumla ya kilometa 20.9 na huduma ya mabasi inaendelea.

Kufuatia kukamilika kwa Awamu ya Kwanza ya BRT (Bus Rapid Transit), Serikali ya Awamu ya Tano  imeanza maandalizi ya  utekelezaji wa Awamu ya Pili, Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne ya BRT Jijini DSM. Awamu ya Pili ya BRT itahusisha barabara za Kilwa, Kawawa na Chang'ombe zenye urefu wa kilometa 20.3 pamoja na flyovers za Chang'ombe na Uhasibu. Awamu ya Tatu ya BRT itahusisha barabara za Azikiwe, Bibi Titi, Uhuru na Nyerere zenye urefu wa kilometa 23.6 kutoka katikati ya Jiji la DSM hadi Gongo la Mboto. Aidha, Awamu ya Nne ya BRT itahusisha barabara za Ali Hassan Mwinyi, Sam-Nujoma na Bagamoyo zenye urefu wa kilometa 25.9 kutoka katikati ya Jiji la DSM hadi Tegeta.

Miradi mingine mikubwa ya barabara na madaraja inayotekelezwa Jijini DSM na Serikali ya Awamu ya Tano ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni pamoja ujenzi wa Flyover ya TAZARA, ujenzi wa barabara za juu (Interchange) katika makutano ya Ubungo, ujenzi wa Daraja jipya la Selander na ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam - Chalinze kwa kiwango cha Expressway.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com