Kufuatia
mabadiliko yaliyofanywa na Bunge katika sheria za usimamizi wa
rasilimali nchini, ongezeko la mrabaha unaotarajiwa kulipwa serikali
uliongezeka kutoka katika asilimia 4 iliyokuwa katika sheria za zamani.
Katika
kuonyesha kukubaliana na mabadiliko hayo, Kampuni ya uchimbaji madini
nchini ya Acacia imekubali kuilipa serikali mrabaha wa asilimia 6
unaoendana na sheria mpya zilizoanza kutumika mwezi huu mwanzoni baada
ya kusainiwa na Rais Julai 5.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo inaeleza kuwa, ili
kuepuka mkanganyiko au mvurugano zaidi kwenye kazi zao katika siku za
usoni, watatimiza matakwa yanayohitajika katika ongezeko la mrabaha wa
katika madini ya dhahabu, fedha na shaba la asilimia 6.
0 comments:
Post a Comment