Mradi wa ufatuaji wa matofali ya zaidi ya elfu Thelathini yatakayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wilaya ya Ilemela umeanza rasmi kutekelezwa baada ya kuzinduliwa mapema wiki hii na Mbunge wa jimbo hilo Mheshimiwa Daktari Angeline Mabula unaotekelezwa kata ya Buswelu ukijumuisha vijana kutoka kata mbalimbali kwa ufadhili wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC ukishirikisha Taasisi ya The Angeline Foundation na Manispaa ya Ilemela
Akizungumza katika eneo la mradi msimamizi wa mradi huo ndugu Michael Selestine amesema kuwa zoezi la utekelezaji wa mradi linaenda vizuri ambapo vijana wamekuwa na uwezo wa kufatua zaidi ya tofali 550 kwa siku huku akifafanua changamoto zinazowakabili kambini hapo
‘… Kwa ujumla zoezi linaenda vizuri, Kazi inafanyika kama ilivyokusudiwa na tunategemea kumaliza kwa wakati tukizingatia ufanisi zaidi isipokuwa tunakabiliwa na changamoto ya namna ya upatikanaji wa maji, Maji yamekuwa changamoto kubwa sana kwa upande wetu yanapatikana maeneo ya mbali si hapa jirani ila vijana wanajitahidi kwakweli mana kwa siku ya jana tu tumeweza kufatua zaidi ya tofali 550 na hapo tumechelewa kuanza naamini tukianza mapema na maji yakapatikana tutazidi kiwango hicho …’ Alisema
Aidha amewasihi wananchi wa maeneo jirani mradi unapotekelezwa kutoa ushirikiano kuhakikisha mradi unafanikiwa nah ii ni kwa maslahi ya wengi si mtu binafsi
Kwa upande wao vijana wanaoshiriki utekelezaji wa mradi huo akiwemo Irene Misana kutoka kata ya Buswelu B ameshukuru uanzishwaji wa mradi huo ambao mbali na kusaidia jamii lakini pia unawaongezea kipato kinachowakwamua kiuchumi na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula na Manispaa ya Ilemela kwa kuwafikiria wananchi wake hasa vijana wananokabiliwa na changamoto ya tatizo la ajira
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
08.06.2017
0 comments:
Post a Comment