Na; Ramadhani Shabani
Ndugu Mtanzania Ni Tumaini Langu Wewe Ni Buheri Wa Afya Na Unaendelea Vyema Na Utekelezaji Wa Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi Tu!Kwa Kufanya Kazi Kwa Bidii Na Weledi Mkubwa Kabisa.
Ndugu Mtanzania Hapo Siku Ya Jana Bunge La Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Liliendelea Na Shughuli Zake Ambapo Kama Ilivyokuwa Kawaida Yake Siku Ya Alhamis Ktk Kipindi Cha Asubuhi Kuwa Kuna Kuwa Na Fursa Kwa Waheshimiwa Wabunge Kumuuliza Maswali Mbalimbali Ya Kisera Mhe Waziri Mkuu Na Kupata Majibu Ya Serikali Papo Kwa Papo.Sasa Ktk Siku Ya Jana Moja Kati Ya Waheshimiwa Wabunge Waliopata Fursa Ya Kumuuliza Mhe Waziri Mkuu Maswali Ya Papo Kwa Papo Ni Pamoja Na *Mhe Ritta Kabati*Ambaye Aliuliza Swali Lake Kama Ifatavyo.
Mhe Spika Nichukue Fursa Hii Kukushukuru Sana Nami Kwa Kunipa Nafasi Hii Ya Kumuuliza Swali Mhe Waziri Mkuu.Mhe Spika Mimi Ni Mbunge Ninaetokea Ktk Mkoa Mmoja Wapo Wa Kilimo Sasa Mkoani Kwangu Iringa Msimu Wa Mvua Zilizopita Tulilima Na Tukapata Chakula Kingi Cha Kutosha Mbaka Na Ziada Ya Kuweza Kuuza Chakula Hichi Nje Ya Nchi Tukapata Pia Lakini Sasa Kumekuwa Na Agizo Kutoka Serikalini La Zuio La Uzaji Wa Mahindi Haya Nje Ya Nchi,Sasa Mimi Nilikuwa Napenda Kufahamu Utekelezaji Wa Agizo Hili Upoje Na Ni Nini Mpango Wa Serikali Juu Ya Hili Zuio!.
Swali Hili Linapata Majibu Kutoka Kwa *Mhe Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa* Ambaye Aliendelea Kusisitiza Ktk Kauli Yake Na Msimamo Wa Serikali Ambao Aliutoa Ktk Akiwa Mgeni Rasmi Ktk Swala Ya Eid Iliyosaliwa Kitaifa Mkoani Kilimanjaro Juu Ya Uuzaji Wa Chakula Hususani Mahindi Nje Ya Nchi,Mhe Waziri Mkuu Alisema Historia Ya Nchi Yetu Ktk Msimu Uliopita Wa Kilimo Ktk Upataji Wa Mvua Haukuwa Mzuri Kabisa Hivyo Kuna Maeneo Haya Kabisa Chakula Cha Kujitosheleza Akiitaja Mikoa Hiyo Kuwa Ni Maeneo Ya Mwanza Na Geita Ambako Mazao Yalikauka Kutokana Na Kukosa Mvua Ya Kutosha Na Hivyo Hizo Ndio Sababu Ambazo Zimeifanya Serikali Kuzuia Uuzaji Wa Chakula Nje Ya Nchi.
Mhe Waziri Mkuu Alisema Lakini Pia Historia Na Tabia Za Watu Wetu Pia Zimebadirika Kwani Kwa Sasa Mahindi Yamekuwa Yakitumika Sana Kwa Wingi Sababu Ugali Umekuwa Chakula Pendwa Na Watu Wote Tofauti Na Zamani.
Akiendelea Kutoa Majibu Ya Swali Hilo La Mhe Mbunge Wa Viti Maalum CCM Mkoa Wa Iringa Ndugu *Ritta Kabati*Mhe Waziri Mkuu Alisema Kwamba Kwa Sasa Zuio La Kusafirisha Mahindi Nje Ya Nchi Lipo Pale Pale Na Huo Ndio Msimamo Wa Serikali Na Labda Tusafirishe Unga Tu!Kwa Kuruhusu Mahindi Hayo Yasagwe Humu Ndani Hili Mabaki Ya Pumba Yabaki Ndani Kwa Ajili Ya Mifugo Yetu Sambamba Na Kusaidia Kuongeza Ajira Kwa Vijana Wetu Kutokana Na Kuongezeka Shughuli Za Ufungaji Na Upakiaji Wa Unga Huo Kuelekea Nje Ya Nchi Lakini Sio Usafirishaji Wa Mahindi Hayo Na Kila Kitu.
*Mhe Ritta Kabati* Amekuwa Akithamini Sana Mchango Wa Wakulima Wa Nchi Hii Na Haswa Wanaotokea Mkoani Kwake Iringa Kwa Kuakikisha Hawadhuriki Kwa Namna Yoyote Na Maagizo Ambayo Yamekuwa Yakitolewa Na Serikali Kwani Amekuwa Akiyaombea Muongozo Kila Siku Ili Kuweza Kupa Ufafanuzi Wa Maswali Ambayo Wananchi Wake Wanaweza Wakawa Nayo Zidi Ya Maagizo Ya Serikali.
CCM Mpya Na Tanzania Mpya Ni Matokeo Taraji Kwa Kila Mtanzania Kutoka Kwa Viongozi Makini Na Wazalendo Walioamuwa Kuwatumikia Watanzania Kwa Dhati Kwa Kusimamia Maslahi Ya Wengi Kwa Kukomesha Unyonyaji Wa Rasilimali Za Taifa Na Mafisadi Wachache.
0 comments:
Post a Comment