METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 24, 2017

Halmashauri Handeni yaagizwa kufuata kanuni za manunuzi

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, kufuata kanuni za manunuzi na kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepuka kutengeneza hoja zinazoweza kuzuilika.

Alisema hayo jana kwenye kikao cha Baraza la Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Alisema manunuzi yote yanayofanyika, yanapaswa kuwa na vielelezo halali ili kuepuka kutengeneza hoja ambazo zingeweza kufutika.

Alisema hoja ya kukosekana kwa vielelezo, halmashauri ichukue hatua kwa watendaji watakaohusika, ambao wanatumia mianya kujinufaisha wenyewe. Aliongeza kuwa, fedha zinazoletwa ni muhimu zikatumika kwa wakati, kwani mahitaji ya wananchi ni mengi na makubwa ili kuepuka bakaa. Zibaki fedha ambazo hazikuletwa kwa wakati.

“Wekeni utaratibu wa kuhakikisha kila vikao mnavyokaa hususani kamati ya fedha mnajadili kiasi cha fedha kilichopo kila kwenye akaunti ili kujua matumizi yake kuepuka bakaa zinazoweza kuzuilika, wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa fedha hizo zinazoletwa na Serikali,” alisema Shigella aliyetaka hoja za malipo kwa watumishi hewa zisijirudie kwa kuhakikisha watumishi wote wanaokuja wanahakikiwa na kulipwa fedha kwa uhalali.

CREDIT: HABARI LEO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com