Mtandao huu ulipowasiliana na Dk. Kigwangalla ambaye yupo Bungeni Mjini Dodoma, alibainisha kuwa, katika kupigania maslai Taifa ataendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli mwanzo mwisho kwani ni moja ya matunda ya nchi yoyote ile Duniani, kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali za nchi, hivyo akiwa Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo bila kuchola. "Tulipambana na tunaendelea kupambana. 2013/4 Nilipambana na kudai haki kwa wachimbaji wadogowadogo na wale waliokuwa wakitunyonya katika migodi yetu, ikiwemo mgidi wa Resolute uliojulikana kama Nzega Golden Pride Project. Tulipambana tulibezwa na hata kulala mahabusu kwa kupambana na rasilimali zetu, leo hii tumepata kiongozi mkuu mwenye uchungu na taifa ili, lazima tumuunge mkono" alieleza Dk. Kigwangalla kwa njia ya simu na mtandao huu. Tazama VIDEO la tukio lingine la Dk. Kigwangalla alivyosimamia masuala ya risilimali Bungeni:
Ujumbe wake huo..
Baadhi ya maoni ya watu
Dk. Kigwangalla akiwa ametiwa nguvuni wakati wa kusimamia haki ulinzi wa migodi jimboni kwake, Nzega, Mkoani Tabora.
Dk. Kigwangalla
0 comments:
Post a Comment