Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia Leo Tarehe 10/04/2017 maeneo ya milimani Zimesababisha adha kubwa kwa wasafiri wa Barabara kuu ya kutoka Korogwe kuenda Moshi ambapo ilizoa udongo mwingi na miti na kuziba Barabara na udongo huo kupelekwa eneo la Barabara kuu.
Mvua hizo zilianza majira ya SAA 4.30 usiku mpaka SAA 6 usiku.
Hata hivyo Magari hayakuweza kupita mpaka ilipofika SAA 1.30 baada ya kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Same kwenda eneo hilo na kushirikiana na wananchi kupunguza kifusi ili magari yaweze kupita.
Kamati hiyo ya ulinzi na usalama ilifika eneo la tukio mnamo SAA 9.00 usiku ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Senyamule.
"Serikali imeshaagiza greda kwa ajili ya kusogeza udongo huo ili kurudisha Huduma hii ya Barabara katika hali yake ya kawaida hivyo matarajio yetu Wakati wowote kuanzia sasa greda hilo litafika, hivyo Tunawapa pole kwa adha mliyoipata"
"Lakini tunashukuru pia tumeweza kutatua tatizo ndani ya masaa 6 tu na Tunawatakia safari njema" Alisema Mhe Senyamule
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Kilimanjaro alifika eneo hilo na kuendelea kusimamia kazi zinazoendelea. Pia kuona namna ya kuliboresha eneo hilo lisiathirike na mvua.
0 comments:
Post a Comment