METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, April 13, 2017

MKURUGENZI UBUNGO ATOA POLE MSIBA WA BABA MZAZI WA SOPHIA KAYOMBO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo Alhamisi April 13, 2017 amejumuika na waombolezaji Kutoa pole kwa Kaimu Mkuu wa Idara ya TEHAMA Manispaa ya Ubungo Bi Sophia Kayombo aliyefiwa na Baba yake Mzazi Mzee Christian Chrisostom Kayombo April 11, 2017 katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.
Mkurugenzi Kayombo ameisihi familia hiyo kuwa na umoja na mshikamo katika kipindi hiki kigumu sambamba na kujiandaa sawia kuelekea mazishi ya Mzee huyo.

Mzee Kayombo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari na matatizo ya Moyo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu mwaka 1998 ambapo mpaka mauti inamkuta alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha Mzee Kayombo alizidiwa Jumatatu ya Tarehe 3/4/2017 ambapo alipelekwa katika Hospitali ya Rabiansi-Tegeta ambapo Siku tatu baadae alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipopatiwa matibabu kwa zaidi ya wiki moja.
Mzee Kayombo ameacha mke na watoto saba, atazikwa kuzikwa Jumamosi Tarehe 15/04/2017 katika maalumu lililotengwa na familia nyumbani kwake Mtaa wa Kiluvya Kwa Komba, Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Mzee Christian Chrisostom Kayomboalizaliwa Mkoani Ruvuma Mwaka 1948 na mpaka mauti inamkuta alikuwa na umri wa miaka 69.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com