METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 5, 2017

ALIYEKUWA BALOZI WA KOREA NCHINI AMTEMBELEA MBUNGE WA ILEMELA

Aliyekuwa Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania kuanzia mwaka 2009 hadi 2012 Mheshimiwa Balozi Kim, Young-hoon amemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziriwa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Daktari Angeline Mabula lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano baina ya Ilemela na Miji rafiki ya nchini Korea,  Kufungua zaidi fursa za Uwekezaji baina ya nchi hizo na utekelezaji wa miradi yote ya kimaendeleo inayotaraji kuanza  Jimboni humo muda wowote kutoka sasa.

Mbali na Balozi huyo Timu ya Uwekezaji ijulikanayo kama KICOT inayojumuisha waTanzania na Wakorea imeambatana na Balozi huyo katika Ziara hiyo huku ikimjumuisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Ilemela Ndugu John Wanga,  Ndugu Son, Ndugu Kim,  Ndugu Lee Kwang Se,  Ndugu Lee Jae-Yong na Ndugu David Mabula .

Aidha ugeni huu unataraji kuwasili jijini Mwanza,  Ilemela mapema jioni ya leo kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo kufuatia kusainiwa kwa mikataba mbalimbali ya miradi ya shughuli za maendeleo mapema mwishoni mwa mwaka jana.

Ilemela ni yetu, Tushirikiane kuijenga

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
05. 04. 2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com