Mbunge
wa Chalinze Mkoa wa Pwani, Ridhiwani Kikwete amehojiwa kwa muda wa saa
tatu na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Ridhiwani
Kikwete alitajwa katika orodha ya majina 97 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda aliyakabidhi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
Kiongozi
huyo alihojiwa Jumatatu Machi 6, 2017 ambapo alifika katika ofisi hiyo
majira ya 5:09 asubuhi akiwa amefuatana na watu wengine watatu.
Ridhiwani
Kikwete baada ya kufika ofisini hapo alipelekwa kwenye chumba maalumu
cha mahojiano ambapo alihojiwa kwa saa tatu ambapo inaelezwa kuwa
alibainika kuwa si muuzaji wala mtumiaji wa dawa hizo, lakini tatizo ni
rafiki zake ambao yupo karibu nao.
Katika
taarifa yake aliyoitoa Jumanne hii, Ridhiwani amesema ameshukuru kuona
haki imetendeka katika sakata hilo lililokuwa likimkabili.
“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika Instagram na kuongeza.
“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika Instagram na kuongeza.
“Tuunge mkono juhudi hizi. Tuunge mkono hatua zinazochukuliwa ili kuokoa vijana wetu na kulinda nguvu kazi ya Taifa #vitadhidiyaMadawa #magufulinikazitu #tanzaniakwanza #miminikazitu #chalinzenikazitu,”
0 comments:
Post a Comment