METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 29, 2017

POLEPOLE ATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM Ndg Humphrey Polepole akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki

Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. John Pombe  Magufuli, leo tarehe 29 Machi 2017 ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Kikao cha Kamati Kuu kimepokea taarifa ya Mchakato wa wanachama na makada wa CCM wanaoomba ridhaa na dhamana ya kuwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

Wajumbe wa Kamati Kuu wametafakari kwa kina wa wameridhishwa na uwazi wa mchakato mzima na namna ambavyo chama kimeonesha demokrasia pana, komavu na shirikishi. Katika mchakato huu jumla ya wanachama na makada 450 walijitokeza, wanawake wakiwa 93 na wanaume 357, wengi wakiwa na elimu ya kuanzia Chuo na Chuo Kikuu.
Chama cha Mapinduzi katika kuzingatia Usawa wa wanawake na wanaume, imefanya uteuzi wa wana CCM 12 kwa mchanganuo wa Bara Me(4) na Ke(4) na Zanzibar Me(2) na Ke(2) ambao majina yao yatawasilishwa Bungeni kwa Uamuzi wa mwisho. Pia chama kimewapa Pongezi sana wana CCM wote ambao wameomba ridhaa

WALIOPATA UTEUZI KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM) ILI KUOMBA RIDHAA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

TANZANIA BARA
WANAWAKE
1.Zainabu Rashid Mfaume KAWAWA
2.Happiness Elias LUGIKO
3.Fancy Haji NKUHI
4.Happiness Ngoti MGALULA

WANAUME
1.Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
2.Adam Omari KIMBISA
3.Anamringi Issay MACHA
4.Charles Makongoro NYERERE

TANZANIA ZANZIBAR
WANAWAKE
1.Maryam Ussi YAHYA
2.Rabia Abdalla HAMID

WANAUME
1.Abdalla Hasnu MAKAME
2.Mohamed Yussuf NUH
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com