Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali(CAG) kuchunguza ukusanyaji mapato ya Shirika la Ndege
Tanzania(ATCL)
Ameyasema
hayo jana alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.
“Nitamuagiza
CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili
kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” alisema Majaliwa.
Alisema
kuwa Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo
amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa
manufaa ya Taifa.
Pia
aliwataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa
mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia
upotevu wa mapato hayo.
Katika
hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo
la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.
Aidha,
Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia
ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
0 comments:
Post a Comment