Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho (kushoto)
akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine
Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.
Aloyce Nzuki wakishiriki Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti
wa Bonde la Ziwa Victoria lililomalizika jana jijini Mwanza.
Mwakilishi wa magazeti ya Uhuru na
Mzalendo wa Jijini Mwanza, Bi. Dorah Michael (kushoto) akipata maelezo
mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya
ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria jana jijini
Mwanza.
Bi. Joyce Kasebela akipokea cheti cha
shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Bonde la Ziwa
Victoria, ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson
Lwenge baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwa mmoja
wa wadhamini wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde
la Ziwa Victoria lilimalizika jana jijini Mwanza.
:Bi. Joyce Kasebele wa Mamlaka ya
Viwanja vya ndege Tanzania (katikati) akiwa na washiriki wenzake kwenye
Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa
Victoria, lililofikia tamati jana jijini Mwanza.
Bw. Prenanning Pamer mkazi wa Mwanza
akipata ufafanuzi wa masuala ya mazingira ndani ya viwanja vya ndege,
kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki wa
Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa
Victoria, yaliyomalizika jana jijini Mwanza.
Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Jiji la
Mwanza, Bi. Esther Madale (kulia) akiwa na Bi. Joyce Kasebele wa
Kitengo cha Mazingira cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali katika Kongamano la Mazingira la
Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria. Kongamano hilo
lilifanyika Jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment