METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, January 17, 2017

DC NDEJEMBI ASEMA TAIFA HALINA NJAA NA HALITAKUMBWA NA NJAA!


Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, 


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deogratius Ndejembi leo mapema, ametembelea Maghala ya Kuhifadhia Nafaka katika soko la kimataifa Kibaigwa. DC Ndejembi amekagua Maghala hayo ili kujiridhisha na takwimu za uhifadhi wa chakula katika wilaya ya Kongwa.

"Kibaigwa ni Soko Kuu la kimataifa la Nafaka Nchini na kuna Maghala yakuhifadhi nafaka ambayo husambazwa nchi nzima na nchi za jirani. Akizungumza na uwongozi wa Soko hilo kubwa, DC alisema.

"Nimekuja kujua kama kweli kuna Ujazo wakutosha ktk Maghala yetu, Nimeona kuna Chakula cha Kutosha na hakuna haja yakusikiliza maneno ya hao wanaotaka kutia Hofu watanzania yakuwa Eti Taifa linanjaa na litakumbwa na Njaa kwa kiwango cha aina yoyote".

Wanachi wa Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa Ujumla Ondoeni Shaka Hakuna Njaa kwasababu chakula kipo. Na Wanasiasa Acheni Kupotosha Wananchi na kuwatia Hofu.
Mbali na hayo alizidi kufafanua akasema Kuna Hifadhi kubwa sana ya Nafaka na inazidi kutoka kuelekea maeneo mbali mbali Nchi, kama kuna mwenye uhitaji wa Mazao ya nafaka Aje Kibaigwa Kongwa atanunua Mazao Tani atakazo.

DC Ndejembi amesema "Kongwa kuna Vijiji kama HembaHemba, Ngomai, Kibaigwa , Mkoka na Mlali Vijiji hivi vina Akiba yakutosha ya Mazao ivo kwanini Mkuu wa Wilaya niseme kuna Njaa?
Alimalizia Mazungumzo yake ametoa wito kwa Watanzania kuwa Makini na Wafanya Biashara ambao hucheza dili za kuuza Mazao na wamezoea kuishi kwa kupewa Vibali vya serikali kwa kununua Mazao kwa bei nafuu kisha kuwauzia Watanzania kwa bei ya Juu! Lakini wamekuwa wakiishi kwa kuanzisha Matatizo ili kutumia Fulsa hiyo kujinufaisha wao.

DC Kasema Watanzania wawe makini sana pia na Wanasiasa ambao wameshaanza kupita nakuwadanganya kuwa Taifa halina Chakula na wao watawaletea Chakula huo ni uwongo mtupu.
Naomba mfahamu kuwa Mh Rais na sisi wasaidizi wake Bado hatujashindwa kulihudumia Taifa hili.

 Aliyasema Ndejembi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa alipokuwa Kibaigwa katika Maghala yakuhifadhia Vyakula.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com