Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mazingira na Muungano January Makamba amesema kuwa mpango wa serikali
ni kuwa na vyanzo vingi vya uzalishaji umeme ili kuwa na vyanzo vya
nchi endelevu na kuunga mkono juhudi za benki ya Dunia kuzalisha umeme
wa upepo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Makamba amesema hayo wakati wa
Kongamano la wadau wa Nishati ya umeme walipokutana kuzungumzia
matumizi ya Nishati ya umeme inayozalishwa kwa njia ya upepo
itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa na mfumo huo utawasaidia
wananchi wa Singida .
“Kwa kuwa umeme huo utazalishwa kwenye
maeneo ya vijijini, wananchi wanatakiwa kupata umeme kwa bei rahisi
kulingana na uchumi wao na sio kuuziwa umeme kwa bei juu, na zaidi
Wizara yake inapenda kuweka wazi kuwa huu mradi una faida kubwa sana
kulingana na mfumo wa nchi ulivyo,”amesema Makamba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki Six Telecoms, Rashid Shamte
amesema kuwa mfumo huu wa gridi ndogondogo una faida kubwa sana kwa
wananchi kwani asilimia kubwa kulingana na ripoti ya benki ya dunia
wananunua umeme wa bei nafuu kwahiyo serikali imekubaliana na kampuni
yetu na imeweza kukubali kuwa mradi huu una tija na utasimamiwa na
serikali yenyewe kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida pamoja na
Halmashauri.
Kwa upande wa Wizara ya Nishati na
Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amewataka wawekezaji
hao kuuza umeme kwa bei rahisi kwani mara nyingi mipango ya serikali
imekuwa haiendani na mikakati ya wawekezaji kwahiyo wanategemea kuona
kuwa mradi huu uwe nafuu ya wananchi wa vijijini kupata umeme kwa bei
rahisi.
0 comments:
Post a Comment