(Kulia) ni Chief
Mrindoko Babu Mwidadi Mwenyekiti Taifa-Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) alipozuru ofisini kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Bondeni Mhe Mbonyo
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Muhammad Shaban(Aluta.D), ambaye ni Katibu Msaidizi-Mawasiliano ya Mwenyekiti Taifa, Makao Makuu imeeleza kuwa ASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA (AWAMATA) Ilipata usajili wa kudumu mnamo tarehe 22/12/2015 na tukapatiwa usajili ooNGO/08343 Na sasa KAZI zote zitafanyika kwenye office ya Mwenyekiti Taifa na hapo ndipo kutakuwa na Makao Makuu ya AWAMAT, Ofisi hivyo ipo Mtaa wa Mbuyuni Kata Bondeni Tembo Road /Manyema Street.
Katika kipindi hiki pamoja na kuwa Asasi imeanza tu na hasa tukizingatia Asasi haina wafadhili lakini iliweza kufanya machache hasa kwa kushirikiana na kundi la Watoto ni Amana (Friends of Fatema)
Kukabidhi tanki la maji kwa watoto kule Mtwara
Kukabidhi tank ya maji na nguo Kibaha
Kukabidhi
matunda, na mswaki,chanuo,kopo la kuhifadhia chakula na mengineyo kwa watoto
wenye saratani pale Muhimbili
Kukabidhi
tank ya maji, nguo, kofia maalulum, kufanya fumigation, vyombo vya jikoni na
mengineyo katika kambi ya kulea watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija
huko Shinyanga
Kituo cha watoto wenye Utindio wa Ubongo
Rombo-Tank la maji lenye lita 500.
Asasi ya Wazalendo na Maendeleo na Tanzania"AWAMATA" inawashukuru wote waliofanikisha tuliyofanya kwa pamoja hasa kundi la Watoto ni Amana (Friends of Fatema) na wazalendo wote na tunatumaini ya ushirikiano zaidi hapo mbeleni kwenye kazi za kizalendo kwa namna mbalimbali.
Kwasasa Asasi inahamasisha watu kuweka oda na kulipia Tshirt za Asasi ambazo zitakuwa sare zetu wakati wa shughuli za kizalendo
0 comments:
Post a Comment