
Balozi Hemed Mgaza, wakati anaapa baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia.
MAONYESHO ya biashara na Utalii yaliyoandaliwa nchini Saud Arabia katika Mji wake Mkuu wa Riyadh, yamefanyika wiki iliyopita huku Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikionekana kung’ara baada ya wageni wengi kupendezwa na bidhaa zilizokuwa zinaonyeshwa katika banda la Tanzania.
Katika maonyesho hayo ambayo bidhaa mbalimbali zilionyeshwa ukiwamo eneo maalum la mlima Kilimanjaro, nguo za Kitanzania na viatu pamoja na bidhaa nyingine muhimu zilizoonekana kuwapendeza wengi waliohudhuria maonyesho hayo.

Akizungumza
katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia,
Mheshimiwa Hemed Mgaza, alisema kwamba wananchi wengi waliohudhuria
maonyesho hayo walionekana kuvutiwa zaidi na nchi ya Tanzania kutokana
na vivutio vyake.
Alisema
hali hiyo imekuja kutokana na aina ya bidhaa zilizoonyeshwa pamoja na
ubunifu wa kutangaza bidhaa zao na nchi kwa ujumla, wakiamini kuwa
utachochea wageni wengi wa kutoka nchini hapa kwenda kutembelea nchini
Tanzania kwa mambo mbalimbali.

“Binafsi nimefarijika mno kutokana na wenyeji kuandaa maonyesho haya na kutuaalika Watanzania ambao watumishi wa ofisi yangu pamoja na mimi mwenyewe wote tulihakikisha kwamba tunayatumia vizuri kutangaza nchi yetu Tanzania.
“Tumewahakikishia kwamba mbali na nchi yetu kujawa na vivutio vingi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, lakini bado tumejawa na amani kiasi kwamba unapokuwa kwenye ardhi ya Tanzania huna sababu ya kuwa na wasiwasi wowote kwa sababu wananchi wake wanaishi kwa upendo,” alisema Balozi Mgaza.
0 comments:
Post a Comment