Na Alex Mathias,Dar es salaam
Timu ya
African Lyon imeharibu sherehe za Simba katika uwanja wa Uhuru jijini
Dar es salaam baada ya kuwatandika goli 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya
Tanzania bara na kuvunja mwiko wa wekundu wa Msimbazi kucheza bila
kufungwa.
Kwa
matokeo hayo yameifanya Lyon kufunga pazia la mzunguko wa kwanza kwa
ushindi mnono na Simba walikuwa wamecheza mechi 13 bila kupoteza hata
mchezo mmoja msimu huu.
Aliyepeleka
kilio Msimbazi ni kinda la zamani la Yanga B,Abdallah Msuhi dakika za
majeruhi 90 baada ya uzembe wa beki pamoja na kipa wa Simba
kujichanganya na kumkuta mfungaji katika nafasi nzuri na kuipandisha
Lyon nafasi ya tisa wakiwa na pointi zao 17.
Licha ya
kufungwa Simba inabaki kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 35
na mchezo wao wa mwisho wa kufunga mzunguko wa kwanza wanaenda kumaliza
mkoani Mbeya dhidi timu ya Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa uwanja wa
Sokoine siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment