Mchezaji
wa Simba Shiza Kichuya akishangilia huku akiwa amebebwa na Laudit
Mavugo mara baada ya kuifungia timu yake ya Simba goli katika dakika
ya 67 kwenye kipindi cha pili cha mchezo wa ligi kuu ya Vodacom katika
uwanja wa Uhuru wakati Simba ilipocheza na timu ya Azam FC jana jijini
Dar es salaam , Katika mchezo huo Simba imetoka kifua mbele kwa kuibuka
na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam FC.
Wachezaji
hao Walishangilia goli lao na kukimbilia mbele ya bango la picha ya
mchezaji aliyekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo Marehemu Patrick
Mafisango aliyepoteza maisha kwa ajali ya gari jijini Dar es salaam na
kusafirishwa nchini kwao DRC Congo, ambako alipumzishwa katika nyumba
yake ya milele akiwaachia majonzi makubwa mashabiki wa Simba kutokana
na umahiri wake katika kucheza mpira ambao uliisaidia na kuipa mafanikio
klabu hiyo.
Mchezaji
wa Simba Laudit Mavugo akishangilia na wenzake mbele ya picha ya
Marehemu Patrick Mafisango aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu hiyo kama
kumbukumbu yake katika mchezo uliochezwa jana kwenye uwanja wa Uhuru
huku Simba ikiibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Azam FC.
Mchezaji
Ibrahim Ajib wa Simba akichuana vikali na Mchezaji Brce Kangwa wa Azam
FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za Simba ya
Dar es salaam na Azam FC pia ya Dar es salaam.
Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo huo wakati ulipokuwa ukiendelea kwenye uwanja wa Uhuru.
Mchezaji
wa Simba Laudit Mavugo akiwatoka mabeki wa timu ya Azam FC Shomari
Kapombe na mbele na David Mwantika katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
uliochezwa jana kwenye uwanja wa Uhuru.
Mchezaji
wa Simba Laudit Mavugo akiondoka na mpira mbele ya mabeki wa timu ya
Azam FC Shomari Kapombe kulia na David Mwantika kushoto katika mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa jana kwenye uwanja wa Uhuru
Piga nipige ikiendelea wakati wa mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment