Bw Buhari
amekuwa akiwahimiza raia wa nchi hiyo wabadili tabiaRais wa Nigeria
Mohammadu Buhari amemalamu mmoja wa wahudumu wake kwa kuiba sehemu za
hotuba ya Rais wa Marekani Barack Obama.
Sehemu
kadha za hotuba ya Buhari aliyotoa tarehe 8 mwezi huu zilifanana na
sehemu za hotuba ya Obama aliyotoa baada ya kushinda uchaguzi mwaka
2008.
Gazeti la
This Day linasema Bw Buhari, kwenye hotuba yake ya Change Begins With
Me (Mabadiliko Yanaanza Nami), alitumia maneno sawa na yaliyotumiwa na
Bw Obama baada ya kushinda uchaguzi mwaka 2008.
Hotuba ya
Bw Buhari ilisoma: "Lazima tujiepushe na vishawishi vya kurejelea
mapendeleo, ukosefu wa ustaarabu na ukosefu wa ukomavu ambavyo vimekuwa
sumu kwa taifa hili kwa muda mrefu. Tulete moyo mpya wa kuwajibika, moyo
wa kutoa huduma, kujitolea na kujitoa mhanga. Sote, tuungane na kufanya
kazi kwa bidii na kujali, sio sisi wenyewe tu binafsi bali pia kuwajali
wengine.
Bw Obama
alisema hivi mwaka 2008, ingawa nukuu zinatoka sehemu tofauti za hotuba
yake: „Nawasihi tujiepushe na vishawishi vya kurejelea mapendeleo,
ukosefu wa ustaarabu na ukosefu wa ukomavu ambavyo vimekuwa sumu kwa
siasa zetu kwa muda mrefu."
"Kwa
hivyo, hebu tulete moyo mpya wa uzalendo, wa kuwajibika, ambapo kila
mmoja wetu anaamua kuungana na kufanya kazi kwa bidii na kujali sio sisi
wenyewe tu binafsi bali pia kuwajali wengine."
Msemaji wa Buhari Garba Shehu anasema kuwa wale waliohusika wataadhibiwa.
Bw Buhari hatakuwa kiongozi wa kwanza mashuhuri kudaiwa kukopa maneno ya hotuba kutoka kwa mtu mwingine.
Wiki
chache zilizopita, mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump, Melania, alidaiwa kukoma sehemu za hotuba yake
kutoka kwa hotuba iliyotolewa na mke wa Rais Obama, Michelle, mwaka
2008.
BBC
0 comments:
Post a Comment