Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewataka
wananchi mkoani Dodoma kuwa makini kabla ya kununua ardhi kwa
kuhakikisha wamepita kwenye ofisi za serikali ili kuepuka utapeli.
Akizungumza
katika kipindi cha NIPASHE kinachorushwa na Radio One, Mabula amesema
kutokana na serikali kutangaza kuhamia Dodoma, ardhi imeanza kuuzwa sana
hivyo wananchi wawe makini kwa kuzingatia taratibu na wasiishie kwenye
ofisi ndogo za mitaa kwani kama watakuwa hawana ramani wanaweza kununua
eneo ambalo limepangiwa shughuli nyingine.
“Wananchi
waende Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ndiyo itawapa ramani za
viwanja vya maeneo na shughuli ambazo zinaonekana kwenye ramani tofauti
na hapo mtu anaweza kununua ardhi ambayo ni halali na kuepuka ghadhabu
ambayo inaweza kuja kutokea baadaye” Amesema Mabula.
Aidha
hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu CDA, Pascas Muragili alisema tayari
mamlaka hiyo imeshafanya kazi ya kuupanga mji huo hivyo wananchi
watakaotoka katika maeneo mbalimbali wawe makini wasije kuuziwa ardhi
kinyemela jambo ambalo litawaletea usumbufu na kupoteza fedha zao.
0 comments:
Post a Comment