Na PC William-Mpwapwa
Idara ya
usafi na mazingira wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma hii leo imetoa taarifa
ya hatua zilizochuliwa dhidi ya uharibifu wa mazingira kwa barua namba
HW/MPW/M10/20/78 ya 29/02/2016.
Pia ameendelea kutoa ufafanuzi kuhusu kata zisizotekeleza wajibu wao na zenye uharibifu mkubwa wa mazingira kwa barua yenye no HW/MPW/M.10/20/86 ya 17/02/2016, kuwa uongozi husika unatakiwa kuainisha na kuorodhesha waharibifu wa mazingira wote, kuhakikisha wahalifu wote wanafikishwa kwenye baraza la kata kwa hatua za kisheria, kuhakikisha wanapanda miti eneo lililo haribiwa na kuhakikisha kuwa hatua zote za utekelezaji na matokeo yanaifikia ofisi ya usafi na mazingira kabla ya siku 21, alieleza kata hizo ni Chunyu,Mima,Iwondo,Nghambi,Manghaliza,Luhundwa,Chitemo,Massa,Kimagai,Pwaga,Malolo,Wotta,Gulwe,Kingiti,Ipera,Berege,Mlunduzi pamoja na Rudi.
Sambamba na hayo ameeleza changamoto mbalimbali wanazozipata kutoka kwa uongozi wa ngazi za chini yani watendaji wa kata na vijiji kutokuwa na ushirikiano katika kutimiza adhma hiyo.
Hata hivyo WazoHuru imemtafuta kwa njia ya simu mtendaji wa kata na vijiji japo hakuweza kupatikana kuthibitisha jambo hili.
0 comments:
Post a Comment