Baadhi ya
watoto wenye ulemavu wakiwa kwenye picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri
wa Sheria na Katiba, Dokta Asha-Rose Migiro pamoja na viongozi wa FPCT.
Mmoja wa walemavu hao Kashinde Athumani akizungumza jambo.
Katika
mikutano mbalimbali kati ya watoto wenye ulemavu na viongozi wa serikali
wakiwemo wale wanaofanya maamuzi, zimekuwa zikielezwa changamoto
mbalimbali ambapo imebainika Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT)
na ERIKS wamehuisha uwezo wa watoto hao kupaza sauti zao.
Watoto
hao kabla ya FPCT kuanzisha mpango wa kuwasaidia, walijiona kama
waliotengwa lakini sasa angalau wana uwezo wa kupaza sauti zao kwa jamii
inayowazunguka wakieleza changamoto wanazopitia kama wanavyoeleza hapa
chini;
”Kwanza,
sisi watoto wenye ulemevu tumekuwa tukitengwa kwenye mambo mbalimbali
kama vile elimu kutokana na kutokuwepo na walimu maalum, vifaa vya
kufundishia na dhana mbaya juu yetu iliyokuwa imejengeka kwenye jamii.
”Wazazi
wetu walikuwa wakituona sisi kama mzigo au tusio na thamani. Matokeo
yake sasa tumekuwa tukikosa elimu na msaada kutoka kwa familia zetu na
jamii inayotuzunguka, mazingira yanayotufanya tuishie kwenye kuwa
ombaomba.
“Serikali
na mashirika ya misaada katika kipindi cha nyuma walikuwa hawatusaidii
kwa lolote, hawakutilia maanani mahitaji yetu, matokeo yake sasa
tumekuwa tumetengwa kwenye masuala muhimu kama vile elimu na shughuli
mbalimbali za kijamii.
“Hatukuwa
na uwezo wa kutengeneza vipato, ndoto za kuingia kwenye maisha ya ndoa
na kupata watoto hatukuwa nazo. Kimsingi tumekuwa kwenye wakati mgumu
sana. Msaada tuliokuwa tunapata ulikuwa mdogo.
“Sasa
ndiyo tunaona kuwa, kama ndugu zetu wangetupa nafasi za kupata elimu
huenda maisha yetu ya baadaye yangekuwa yenye mwanga lakini tulitengwa
na kuachwa kwenye umasikini,” wanaeleza watoto hao.
Hivyo
watoto Baraza la Watoto Wenye Ulemavu wameitaja FPCT na washirika wake
ambao ni ERIKS kama watu wa pekee ambao wamewafanya wajisikie kuwa nao
ni binadamu kama wengine kwani wamekuwa wakiwasaidia katika kupata elimu
juu ya haki zao za msingi na namna ya kukabiliana na changamoto
wanazopitia. Wasikie watoto hao wanavyowapongeza FPCT na ERIKS.
“Sisi
watoto wenye ulemavu sasa tunajiona tuko salama na tumepata ujasiri na
uelewa juu ya haki zetu hasa baada ya FPCT na ERIKS kuandaa mpango wa
kutusaidia. Wametuunganisha na watoto wenzetu wasio walemavu, kujifunza
juu ya haki za watoto, kujadili haki zetu na changamoto tunazopitia,
kuiamsha serikali na wadau wengine kutusaidia.
“Miradi
mbalimbali iliyokuwa inaandaliwa na FPCT imewafanya wazazi na jamii kwa
ujumla kuona umuhimu wetu kwenye jamii na kujua majukumu waliyonayo
katika kuhakikisha tunaishi maisha salama.
“Na sasa
tunaona mabadiliko makubwa kwani wazazi, wanajamii na walimu angalau
wanajali haki zetu na wanatusaidia katika kukabiliana na changamoto
tunazopitia.
Baraza la
watoto wenye ulemavu mkoa wa Arusha kupitia mwenyekiti wake wameitaka
serikali iweke bajeti kwa ajili ya watoto wenye ulemavu na si kuwaachia
FPCT na ERIKS kama vile ndiyo watu pekee wenye jukumu hilo.
Mwenyekiti
kutoka Mkoa wa Tabora alisema: “Tulishangaa kuona FPCT na ERIKS
wanatuandalia mikutano na viongozi wa wilaya na mikoa kisha kujadili juu
ya matatizo ya kielimu tunayokumbana nayo wakati hilo ni jukumu la
serikali. Ila tunayo furaha kusikia serikali imeahidi kututatulia
matatizo yetu.
Viongozi
wa watoto wenye ulemavu mkoani Rukwa walisema kuwa, baraza lao linafanya
kazi kubwa ya kuwashinikiza viongozi na wafanya maamuzi wengine
kuyatilia maanani mahitaji yao ila tatizo ni kwamba baraza hilo
halikutani mara kwa mara.
Hivyo
jitihada zinahitaji kuhakikisha baraza lao linakutana mara kwa mara ili
kuweza kupata nafasi ya kujadili matatizo yao na changamoto zao mara kwa
mara bila kuwategemea tu FPCT na ERIKS.
Huko
Shinyanga, mwenyekiti wa baraza la watoto anasema kuwa, kumekuwa na
ongezeko la kuripotiwa kwa matukio ya watoto kufanyiwa vitendo vibaya,
na hii ni kutokana na mchango mkubwa wa FPCT na ERIKS ambao waliandaa
mradi mkoani mwao.Kwa hiyo sapoti bado inahitajika ili kuwezesha elimu
itakayosaidia kuongeza uelewa wa watu juu ya haki za watoto inaenea.
Kauli za watoto wenye ulemavu kutoka kwenye mabaraza ya mikoa mbalimbali
Clara Damian (mwenye ulemevu wa macho) kutoka Arusha anasema:
Clara Damian (mwenye ulemevu wa macho) kutoka Arusha anasema:
Kupitia baraza hili nimejua haki zangu. Nimekuwa mshauri mzuri kwa watoto wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi kuwajali na kuwapeleka shule badala ya kuwafungia ndani.
Pia ninao
ujasiri wa kuandaa mikutano na waandishi kisha kueleza mambo mbalimbali
yanayotuhusu kupitia redio na televisheni. Pia naweza kukutana na
viongozi wa serikali na kuwahimiza kuzilinda haki zetu na kutatua
changamoto zinazotukabili.
Emmanuel
Mpozi kutoka Mbeya: “Ninao ujasiri wa kusimama popote na kuzielezea haki
zetu kwenye jamii, na hii yote ni kutokana na mchango mkubwa wa FPCT na
ERIKS.
Imeandikwa na Amran Kaima.
Imeandikwa na Amran Kaima.
0 comments:
Post a Comment