Mabingwa
wa Ligi Kuu ya Tanzania, Yanga SC imefanikiwa kufuzu mzunguko wa pili wa
Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga klabu ya Cercle de Joachim
goli mbili kwa bila na hivyo kuwa na wastani wa goli tatu kwa bila ambao
unaipa Yanga nafasi ya kusonga mbele.
Magoli ya
Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Amissi Tambwe katika dakika ya
tatu baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa na Simon Msuva.
Goli la
pili katika mchezo huo lllifungwa na kiungo wa klabu hiyo, Thaban
Kamusoko katika dakika ya 56 na hivyo kuihakikishia Yanga nafasi ya
kucheza mzunguko wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment