Mapigano
yemeendelea kuripotiwa Syria kinyume na mpango wa amani uliofikiwa kwa
ushawishi wa Marekani na Urusi. Saudi Arabia inatupa lawama kwa serikali
ya Syria kutokuheshimu makubaliano.
Vikosi
vya serikali ya Syria vimeidhibiti barabara muhimu inayoelekea katika
mji wa kaskazini wa Aleppo baada ya kusonga mbele dhidi ya wanamgambo wa
kundi la Dola la Kiislamu IS hivi leo. Kwa mujibu wa shirika
linalofuatilia masuala ya haki za binaadamu la Syria lenye makao yake
mjini London nchini Uingereza, mapambano makali yameendelea kati ya
vikosi vya seriakli na wapiganaji wa kundi hilo katika eneo la kusini
mashariki mwa mkoa wa Aleppo.
Ufanisi
wa serikali ya Syria katika mkoa wa Aleppo kupitia msaada wa
mashambulizi ya kutokea angani ya Urusi na wapiganaji washirika kutoka
Iran na wa kundi la Hezbollah la Lebanon, unakuja katika siku ya tatu ya
utekelezaji mkataba wa kusitisha uhasama kati ya Marekani na Urusi,
ambao hauyajumuishi makundi ya Dola la Kiislamu na Al Nusra Front.
Waziri wa
mambo ya nchi za kigeni wa Saudi Arabai, Adel al Jubeir, aliishutumu
Urusi na serikali ya Syria kwa kukiuka usitishwaji mapigano nchini
Syria. "Kuna uvunjifu wa usitishaji mapigano uliofanywa na vikosi vya
Urusi na utawala wa Syria, na tunashauriana na nchi za kundi
linaloisaidia Syria. Nadhani kujitolea kwa dhati kuuheshimu usitishwaji
mapigano itakuwa ishara muhimu kutoka kwa utawala wa Syria."
Akizungumza
katika mkutano na waandishiwa habari akiwa pamoja na waziri wa mambo ya
nchi za nje wa Denmark, Kristin Jensen, aliyekuwa ziarani mjini Riyadh,
Jubeir alisema kutakuwa na mpango mbadala ikiwa itadhihirika wazi
kwamba rais wa Syria, Bashar al Assad, na washirika wake hawayaheshimu
makubaliano, lakini hakutoa maelezo yoyote.
Kwa
upande wake waziri Jensen alitoa wito kuundwe muungano imara kuongeza
shinikizo la kijeshi kwa utawala wa Assad kusaidia kuvimaliza vita
nchini Syria. "Kuna suluhisho la kisiasa tu kwa tatizo la Syria, vita
vya Syria, lakini suluhisho la kisiasa linaweza kupatikana kupitia
kitisho cha kijeshi, vinginevyo Assad ataendelea na utawala wake wa
kinyama ambapo amewaua maelfu ya raia wake mwenyewe na kuwafanya zaidi
ya nusu ya wakazi kuwa wakimbizi."
Usitishwaji uhasama uambatane na mchakato wa kisiasa
Wakati
haya yakiarifiwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani, Frank
Walter Steinmeier, amesema usitishaji mapigano nchini Syria utaheshimiwa
iwapo utaambatana na mchakato wa kisiasa. "Unaweza kuona katika sura za
Wasyria wakati huu kwamba wasiwasi na matumaini vimekaribiana sana na
bila shaka ni mapema mno kusema kama usitishwaji mapigano utadumu."
Steinmeier
aliyasema hayo jana katika uwanja wa ndege wa Tegel mjini Berlin kabla
kuondoka kwenda Marekani kwa mazungumzo zaidi na waziri wa mambo ya nchi
za nje wa nchi hiyo, John Kerry.
0 comments:
Post a Comment